Umejaribu kuchomoa hard-disk na kuirudishia? Maana kuna uwezekano ikawa imelegea...na pia na fan yake unaisikia ikiwa inazunguka na kupooza?Habari wa weekend wanajamvi!
Naomba msaada wa kuelewa hili tatizo, nina PC hapa EliteBook HP kuanzia jana jioni inaleta maruweruwe.
Nikiwa naitumia inazima ghafla hata kama chaji iko ya kutosha na nimejaribu pia ikiwa direct connected na chaja.
Kimbembe kinakuja ikijizima, kuwaka inachukua muda kidogo na itafanya hivyo mara kadhaa kabla ya kukaa sawa na tatizo kujirudia baada ya muda.
Naomba msaada wa kitaalamu kwa wajuvi wa mambo
Asanteni!
Ishu ya hard-disk unaweza ukalifanyia kazi labda kama ni mgeni ktk masuala ya computer, na pia unaweza ukatafuta tutorial mtandaoni ya namna ya kufungua hard-disk kutoka kwenye pc(jina & model ya pc).Hilo suala la hard-disk sijafanyia kazi ila nadhani fundi ananihusu hapa.