Msaada: Nyuki wamevamia nyumbani kwangu

Msaada: Nyuki wamevamia nyumbani kwangu

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,641
Reaction score
3,659
Wakati nafika nyumbani leo nimekuta NYUKI wamejikusanya kwenye paa la nyumba,

Ni sehemu ya hatari maana kila mtu anapita.

Naomba msaada nitumie njia gani kuwatoa maana nimeona kuwatoa kwa moto haiwezekani.

Au kama kuna dawa ya kuwafukuza naomba msaada. Shukrani

Private geologist
 
Wafuge ndani ya miezi miwili unapata asali unauza inatoka hiyo.

Just for fun

Tafuta pumba ama kitu kingine kinachoweza kutoa moshi kwa muda mrefu halafu choma hapo chini yake
 
subiri jioni mkuu yani hapo usiwaguse, kipindi nasoma secondary tabora ikifika mwezi wa sita ule muda kufunga shule tulikuwa tunafua mabegi yetu na kuyaanika kwenye mitaimbo au kwenye miti, aisee yaani kabla ya kukauka nyuki hao wanazama, tulikuwa tunawaacha ikishafika giza unaenda unachukua begi lako unakung'uta wanatoka wote, hapo subiri giza mkuu, ila kung'atwa utang'atwa tu,
 
Washa moto, moshi wake watakimbia.

Tena ukipata bangi ukanyanganya inakuwa rahisi sana.

Ina maana udogoni hukuwa unarina asali au kula asali za mitini porini????????????????????????????
 
Washa moto, moshi wake watakimbia.

Tena ukipata bangi ukanyanganya inakuwa rahisi sana.

Ina maana udogoni hukuwa unarina asali au kula asali za mitini porini????????????????????????????
Udogoni tulikuwa tunatumia moto, sasa hawa wa kwenye paa kuwatimua na moto ni hatari
 
Washa moto, moshi wake watakimbia.

Tena ukipata bangi ukanyanganya inakuwa rahisi sana.

Ina maana udogoni hukuwa unarina asali au kula asali za mitini porini????????????????????????????
watoto wa mjini hawa ndio wamepelekwa maporini
 
chukua dawa za kupuliza (km Rungu, Expel nk)
vaa net ya kawaida km zile za Bush zitolewazo Clinic halafu tafuta box linalotosha kichwani litoboe,
pulizia hasa hata kopo mbili hakikisha pale kwenye sega unapahamisha
baadaye dawa ikitulia choma vitu vitoe moshi
kuwaita furmigationau Idara ya nyuki inaweza kufika 200,000/
wakati kazi unaiweza mwenyewe
 
Wakati nafika nyumbani leo nimekuta NYUKI wamejikusanya kwenye paa la nyumba,

Ni sehemu ya hatari maana kila mtu anapita.

Naomba msaada nitumie njia gani kuwatoa maana nimeona kuwatoa kwa moto haiwezekani.

Au kama kuna dawa ya kuwafukuza naomba msaada. Shukrani

Private geologist
Chukua lile bua lamlingoti wa mkatani lililokauka ulichome ulemoshi yake usogezee chini ya hao nyuki waliko alafu ulee mrejesho baada ya kazi hiyo
 
picha ya nyuki
6cb86e2e192c46596cc4d5e4cc0e322a.jpg

Hapo kwenye rangi nyeusi nimeshindwa kuwasogelea
 
Sipati picha wakikung'ata mdomo sijui utatoka nje ama utakaa ndani hutoongea na mtu...bado nawaza hapa

Subiria Giza, tafuta mahali unapotaka wadondokee koleza moto upande huo alafu wabonde na mawe watadondokea huko na watakumbana na moto...wataungua wengi na watabaki wachache...watakaobaki watahama usiku huohuo
 
Back
Top Bottom