Msaada: Nitajuaje siku za hatari kwa mke wangu?

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,019
5,436
Satute,

Niende moja kwa moja kwenye mantiki, mke wangu ziku zake za hedhi zimetokea kuvurugika tu, hivo napata mtihani mkubwa sana kujua siku zake za hatari.

Ziku zake za hedhi kwa miezi ya karibuni iko hivi, mwezi wa 5 aliingia tarehe 20, mwezi wa 6 aliingia tarehe 10, mwezi wa 7 aliingia tarehe 10, mwezi wa 8 aliingia tarehe 5 na mwezi wa 9 kaingia tarehe 18.

Kiukweli imeniacha njia panda kubwa sana za kuweza kutambua siku za kuweza kupata mimba kwa kipindi cha nyuma alikuwa akiingia kila tarehe 10 ya kila mwezi wakuu kwa mabadiliko hayo nitahesabu vipi siku zake za hatari?

Ushauri wenu tafadhali.
Nawasilisha

By
Young

Dimaa.
 
Muambie aingie playstore a-download Lady timer Calendar, then ataweka tarehe za nyuma alizoingia period yake.

Akifuatisha hiyo itakua msaada mkubwa sana kwake hata kama siku zake zinavurugika
Thanks mkuu
 
Yaani mfano hiyo ya mwezi huu kaingia tarehe 18 sasa ukihesabu siku 14 utaona siku za hatari itaangukia kwenye tarehe mbili ya mwezi ujao
Hivi haiwezekani mwanamke kuangukia katika tarehe moja kila mwezi?, mfano anaingia kila tarehe 10 ya kila mwezi , afu ukisoma kwenye mitandao wanakwambia katika siku yake ile ya hatari unaadd siku tatu mbele na siku tatu nyuma, kuna ukweli?
 
Itakuwa ameadhirka na madawa ya uzazi wa mpango,cku za nyuma hizi ni zaidi ya matatizo
 
Hivi haiwezekani mwanamke kuangukia katika tarehe moja kila mwezi?, mfano anaingia kila tarehe 10 ya kila mwezi , afu ukisoma kwenye mitandao wanakwambia katika siku yake ile ya hatari unaadd siku tatu mbele na siku tatu nyuma, kuna ukweli?
Mimi tarehe zangu hazieleweki km za mkeo, hizo kuadd siku tatu nyuma na mbele ni Kweli na ndo hata mimi huhesabu ivo
 
Hiyo ni kweli kabisa mkuu
 
Mimi tarehe zangu hazieleweki km za mkeo, hizo kuadd siku tatu nyuma na mbele ni Kweli na ndo hata mimi huhesabu ivo

hahaha hakuna kitu ambacho nilishashindwa km hayo makitu jaman ! mie hazibadiliki hata kidg ila sasa nahesabu fresh tu lakini unajikuta next month huon mp !naudhika sana jaman !sitak kabs kusikia hizi kalenda ! wanangu wote nilienda na kalaenda lakini wapiiii! mie nahisg siku zote kwangu ni danger tu mxiew
 
Dalili ni chuchu zake tu.
Zikianza kuvimba vi chuchu tu SIO maziwa.
Ujue safari ya kwenda mwezini imekaribia
 
hahaha hakuna kitu ambacho nilishashindwa km hayo makitu jaman ! mie hazibadiliki hata kidg ila sasa nahesabu fresh tu lakini unajikuta next month huon mp !naudhika sana jaman !sitak kabs kusikia hizi kalenda ! wanangu wote nilienda na kalaenda lakini wapiiii! mie nahisg siku zote kwangu ni danger tu mxiew
Angalie usituzalie kijiji ndugu yangu ,njia rahisi ya uzazi wa mpango kwa wenye ndoa ni hiyo ya kalenda japo inahitaji mwanaume muelewa sana na anayekusikiliza vinginevyo ni kazi bure, binafsi naitumia sana japo kwa mtoto wangu huyu wa sasa niliishindwa mambo yalibana balaa matokeo yake nna mapacha wa nje na ulezi wake utajutia ulichokifanya na kusema si ungesubiri tu
 
Chukua first day of her last menistruation then count fourteen days. Hiyo siku ya 14 ndio kuna red indicator usiguse kabisa. For precaution usido from day 11.
 
Back
Top Bottom