Msaada: Nisaidieni kwa hili wanaJF

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Nina mpango wa kupeleka matangazo ya Biashara sehemu tatu (3); Radioni, kwenye Luninga (Tv) na kwenye mitandao ya kijamii ya hapa hapa nyumbani (blogs) kama JF.

Sasa Je, kama ni Radio mngenishauri kupeleka matangazo kwenye Radio gani na kwenye kipindi kipi? Kama ni Tv mngenishauri kupeleka matangazo kwenye kituo gani cha TV na kwenye kipindi gani?

Na mwisho kama ni kwenye mitandao ya kijamii ya hapa nyumbani (local) je mngenishauri mtandao gani na kwenye jukwaa au mada gani?

Ahsanteni sana na samahani kwa usumbufu..
 
Natoa mchango wangu kwa SOCIAL MEDIA tuu, kama ifuatavyo:-

1. JF ndiyo namba moja kwa upande wa blogs na website hapa Tanzania

2. Kwenye social media yapo makundi mawili:-

a. Kundi la watu wanaotumia social media kama kwa starehe, ku socialize, n.k e.g Instagram, twiter n.k, wapo wadau kibao mfano ROSE NDAUKA nimeona anatangaza sana kwenye instagram na gazeti lake.

b. Kundi la apps (application za simu) zinazotumika na watanzania kupata huduma mbalimbali k.v kazi, nyumba, usafiri, tickets na suggest Grab! city info Co. (cheki instagram page kupitia ID hii: grabcityinfo) wana apps zinazotumiwa na watu mbali mbali hasa vijana na wageni wa nchi mbali mbali, so ikiwa target customers wako ni vijana na foreign nationals basi hapo ndipo penyewe.

c. Kundi la brokers wa social media. Hawa ni wadau wanafanya matangazo kupitia social media na wateja wao ni makampuni makubwa makubwa tuu, kama vile Voda, Airtel n.k. Ni PM nikupe details zao.

Pamoja
 
Ahsante sana Mkuu...ngoja niwasubirie wadau wengine labda watanisaidia kwenye upande wa Radio na Tv
 
Back
Top Bottom