Msaada: Nina kwikwi kwa wiki mbili sasa, naomba kufahamu dawa yake

Dah!!
Nilimshuhudia rafiki yangu akipata kwikwi siku 3 mfululizo.

Alijaribu kila aina ya maelekezo kama, Kubana pumzi kwa muda then unaachia, ama kuvuta pumzi ndani then unazuia, kunywa maji mengi, kumweleza jambo ambalo litamshtua hasa (Uongo flani) n.k

But haikusaidia, siku nimeenda kumuona nikamuonea huruma, yeye akawa anasema hari yake inasababishwa na mambo ya Ushirikina, nikamwambia pale pale tunaenda Hospital, nikambeba mpaka Hospital, Doctor akaeleza kitaalam Kwikwi inavyosababishwa, akasema kwa lugha rahisi ni pale iliyopo ndani na ile iliyopo nje zinaposhindwa kupishana (Kitendo cha kupumua)

So Kwikwi inatokea pale Hewa ya ndani inataka kutoka nje, na pale pale hewa ya nje inataka kuingia ndani, akasema kitendo cha kunywa maji mengi, kuvuta pumzi, kumshtua mtu n.k vyote vinaweza kusaidia ile hari ya Upumuaji kurudi kawaida, kama Kwikwi ni ya kawaida, akasema pia zipo Dawa, akamchoma Sindano akampa na Vidonge flani akameza, baada ya dakika 5 pale pale tukiwa Hospital Kwikwi ikakata!

Karudi nyumbani mzima, ila kesho yake pia alivyoamka tu Kwikwi ikaanza, cha ajabu Kwikwi ilikata kila akilala na kuanza kila akiamka, akichoma Sindano na Vidonge Kwikwi inaacha kwa siku hiyo, next day inaanza tena!

Baadaye akasafiri bila kuaga mtu, hata mm hakuniaga, akanipigia simu baada ya siku 3 kuwa yupo kwa Mganga na kutaka nisimwambie mtu!

Karudi baada ya week 2 akiwa mzima, na story mingi kadri ya Imani yake kwenye Ushirikina!

(Binafsi natambua Ushirikina upo ila siamini kwenye Ushirikina zaidi ya maombi).

Ushauri wangu kwako kutokana na kuwa Shuhuda, ikifika siku 3 hiyo hari bado ipo, kwanza nenda Hospital huku ukifanya maombi wewe mwenyewe. (Inategemea na imani yako).
Asante sana
 
Habari, kwikwi inanisumbua siku ya pili sasa. Nimekunywa maji mengi, sukari nimeramba lakini bado tuu.
Naombeni msaada

Kwikwi inayodumu zaidi ya saa 48 yahitaji kufatiliwa na mtaalamu wa afya.

Kwikwi ni matokeo ya irritation/muwashawasha kwenye vagus nevu, ambayo hupeleka mawasiliano kwenye diyaflam/diaphragm. Hii husababisha spasm ya kiwambo hicho na ndo kwikwi hutokea.

Matokeo ya irritation ya vagus nevu yaweza kuanzishwa na vitu vingi:

1: Maambukizi au muwasho kwenye njia ya chakula.

2: Matatizo ya figo

3: Matatizo kwenye ubongo

4: Matatizo kwenye sikio

5: Matatizo ya madini mwilini

6. N.k.

NB: Ni vyema kufika kituo cha afya kwa uangalizi wa wataalamu ili kuondoa kisababishi na kwikwi yenyewe.
 
Dah!!
Nilimshuhudia rafiki yangu akipata kwikwi siku 3 mfululizo.

Alijaribu kila aina ya maelekezo kama, Kubana pumzi kwa muda then unaachia, ama kuvuta pumzi ndani then unazuia, kunywa maji mengi, kumweleza jambo ambalo litamshtua hasa (Uongo flani) n.k

But haikusaidia, siku nimeenda kumuona nikamuonea huruma, yeye akawa anasema hari yake inasababishwa na mambo ya Ushirikina, nikamwambia pale pale tunaenda Hospital, nikambeba mpaka Hospital, Doctor akaeleza kitaalam Kwikwi inavyosababishwa, akasema kwa lugha rahisi ni pale iliyopo ndani na ile iliyopo nje zinaposhindwa kupishana (Kitendo cha kupumua)

So Kwikwi inatokea pale Hewa ya ndani inataka kutoka nje, na pale pale hewa ya nje inataka kuingia ndani, akasema kitendo cha kunywa maji mengi, kuvuta pumzi, kumshtua mtu n.k vyote vinaweza kusaidia ile hari ya Upumuaji kurudi kawaida, kama Kwikwi ni ya kawaida, akasema pia zipo Dawa, akamchoma Sindano akampa na Vidonge flani akameza, baada ya dakika 5 pale pale tukiwa Hospital Kwikwi ikakata!

Karudi nyumbani mzima, ila kesho yake pia alivyoamka tu Kwikwi ikaanza, cha ajabu Kwikwi ilikata kila akilala na kuanza kila akiamka, akichoma Sindano na Vidonge Kwikwi inaacha kwa siku hiyo, next day inaanza tena!

Baadaye akasafiri bila kuaga mtu, hata mm hakuniaga, akanipigia simu baada ya siku 3 kuwa yupo kwa Mganga na kutaka nisimwambie mtu!

Karudi baada ya week 2 akiwa mzima, na story mingi kadri ya Imani yake kwenye Ushirikina!

(Binafsi natambua Ushirikina upo ila siamini kwenye Ushirikina zaidi ya maombi).

Ushauri wangu kwako kutokana na kuwa Shuhuda, ikifika siku 3 hiyo hari bado ipo, kwanza nenda Hospital huku ukifanya maombi wewe mwenyewe. (Inategemea na imani yako).
umeshamwaga siri
 
umeshamwaga siri
Siri gani?
Mara nyingi nikiona mtu anasumbuka na jambo flani ambalo nina Uzoefu nalo, huwa naeleza true story nilivyoshuhudia kama ilivyo, bila kupunguza wala kuongeza neno, Then Muhusika atachagua kipi kinaweza kumsaidia!

Coz kwenye habari kama hizi wengi husikia kuwa ikiwa hivi nasikia dawa na hii, but mm nimshuhudia na kushiriki kutoa Msaada, so nimeeleza kwa nilichoshuhudia.
 
Mrejesho; kama nilivyokuja kuomba msaada wa mawazo kutokana na KWIKWI kunishika kwa siku kadhaa
Nilijaribu kila kitu nilichoshauriwa
1. Kunywa maji - ilikuwainasaidia kwa muda tu
2. Sukari - kwa muda
3. Hospital nilikwenda nikapata dawa na vipimo juu lkn iliendelea
4. Matunda (matango) - baada ya kula matango kwikwi ilikata moja kwa moja.
N.B: nilishauriwa nipate muda wa kutosha wa kupumzika tena kwa kuzima simu kabisa. Hii pia ni dawa nzuri.
Mwisho wa siku naweza sema dunia ina mambo mengi.

Asanteni sana kwa ushauri wenu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom