MSAADA: Nimepoteza hati ya kiwanja na sina copy yake

mamitod

JF-Expert Member
May 20, 2015
904
500
Wakuu nawasalimu.
Poleni kwa majukumu ya kila siku pamoja na harakati za kupambana na makinikia yetu.
Naomba nisiwapotezee muda kwa hadithi ndefu. Nimepoteza hati ya kiwanja naomba msaada wa mawazo nini cha kufanya maana sina copy na original ndio imepotea katika mazingira tata. Nafikiri nilisahau bahasha iliyokuwa na fomu hiyo mahali na nilipofuatilia mhusika alikataa kuiona. Toka jana kwa kweli kichwa kinauma tokana na hilo. Nipeni msaada wa njia yo yote utakaonifanikisha kupata hati nyingine tafadhali. Sijui nikaripoti polisi au vipi? Nikienda ardhi kuomba watanikubalia kwamba ni mimi ilihali nilinunua toka kwa mtu? Yaani hiyo hati niliinunua toka kwa mtu na nilikuwa sijabadilisha jina. Wakuu msaada tafadhali. Naomba usijibu cho chote kuliko kunikejeli. Najua wengi humu ni waungwana. Please do the needful, I am in trouble. Ahsanteni
 

kmayunga

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
223
250
Kuripoti polisi ni muhimu na ndiyo cha kwanza kufanya ndiyo huende ardhi kwa ushauri zaidi.
 

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,957
2,000
Mtafte alyekuuzia mfanye mpango wa kupewa nyingne.

Ila hapa kwenye "Hati ya kiwanja" bado namashaka.
 

ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
10,173
2,000
Fanya hivi....mjulishe aliyekuuzia kiwanja kwamba umepoteza hati.....yy aende polisi akaandaliwe loss report .....mkipata loss report nendeni kwa msajili wa hati muombeni awatengenezee hati nyingine.....ovious itakuwa kwa jina la yule aliyekuuzia ....mkifanikiwa ufanye transfer...mkalipe capital gain tax tra ...mchezo umeisha
 

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,681
2,000
Nenda ulipoipatia wakupe copy! I mean, yule aliyekuuzia lazima atakuwa na copy... I hope una mikataba ya aliyekuuzia hata kama bado hujabadilisha jina. Cha muhimu kama ulinunua kwa kutransfer pesa kutoka kwenye akaunti yako kwenda kwenye akaunti yake ushahidi unakuwepo hata akikugeuka...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom