Msaada: Nimepima presha ipo juu

Msaada: Nimepima presha ipo juu

Naxria abdalla

Senior Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
158
Reaction score
281
Habari zenu naomba husika na mada apo juu jana baada ya kujsikia vibaya nikaenda hosptal na kupima baadhi ya magonjwa ila nimekutwa na presha 140/100 nina miaka 32 naomba kueleweshwa njia za kutumia ili kupunguza iyo presha tofauti na kula dawa ahsante
 
Acha kula kula ovyo kama nguruwe, jiepushe na vitu vya sukar ( mihogo, viaz,wali, ugali,ngano) usije mpata mdogo wake pressure ( diabetes mellitus)

Fanya mazoez kunywa maj meng achana na kubet na mademu wasioeleweka

Jipende mwenyew kabla mwanamke

Kula matunda na vyakula ulivoshauriwa
 
Tibu ugonjwa unaokusumbua mzee wangu maana mara nyingi presha inasababishwa pia na ugonjwa mwingine ulionao. Kama una vidonda vya tumbo ama ugonjwa mwingine au ma stress basi yatibu kwanza ndio presha itashuka mkuu.

Pia usinywe energy drinks au kahawa na kunywa maji ya kutosha na kula vitunguu swaumu kwa kutafuna kama utaweza au kata vipande vidogovidogo umeze kama vidonge.

Pole sana na nakuombea uzima na uponyaji katika siku hii ya SABATO.
 
zingatia uzito wako wa mwili kuendana na urefu wako na zingatia pia mlo unaofaa pia epuka msongo wa mawazo.
 
Habari zenu naomba husika na mada apo juu jana baada ya kujsikia vibaya nikaenda hosptal na kupima baadhi ya magonjwa ila nimekutwa na presha 140/100 nina miaka 32 naomba kueleweshwa njia za kutumia ili kupunguza iyo presha tofauti na kula dawa ahsante
Aliekupima umemuacha bila kumuuliza hilo swali unakuja kuuliza huku???? Hivi unapenda uhai wako kweli?? Mbona unafanya mambo ya kitoto akati umri unakutupa mkono? Ishu inahusika na afya yako(life and death) unakuja mitandaoni kutafuta hoja za "How to"???? No wonder vijana tunakufa hovyo sababu ya dharau.. Acha ujinga rudi hosptali.
 
Una kazi?
Pressure katika umri huo kunakuwa kuna jambo linakusumbua stress, hofu kubwa moyoni n.k

Ukipambana na suala linalokupa presha ndipo utatibu presha hiyo. Vinginevyo hata ule mawe. Ndio maana utasikia watu wanakwambia tuliza presha, presha ya nini?

Yaani ili uwe na presha lazima kuna kitu kinaelemea moyo wako.
 
KAKA UNAMILIKI PISI KALI YOUOTE HUO UMRI VIJANA WENGI NI STRESS KUTOKA KWA MADEM, MAMBO YA KIFAMILIA NK, FANYA MAZOEZI KUNYWA MAJI MENGI KUBWA ZAIDI MPENDE MUNGU WAKO MFANYE AWE MSHIKAJI WAKO KUNA MUDA ONGEA NAE NDAANI PEKEE AKO INSHORT MFANYE SWAHIBA WAKO
 
Aliekupima umemuacha bila kumuuliza hilo swali unakuja kuuliza huku???? Hivi unapenda uhai wako kweli?? Mbona unafanya mambo ya kitoto akati umri unakutupa mkono? Ishu inahusika na afya yako(life and death) unakuja mitandaoni kutafuta hoja za "How to"???? No wonder vijana tunakufa hovyo sababu ya dharau.. Acha ujinga rudi hosptali.
Wewe ndo uache ujinga mana ungepita bila kuchangia uwo unaoita ujinga ingependeza sana
Pungua mpaka 44 kata hizo 30 fanya mazoezi punguza kitambi
Ahsante kwa ushaur
 
Maji mengi unayoshauriwa kunywa pia yana shida,wakuambie mengi kiasi gani siyo unajitwisha Lita 5 kwa siku!!

Fanya mazoezi,maji unywe mwili ukihitaji kuna sensor itakujuza ukihitaji maji.
 
Una kazi?
Pressure katika umri huo kunakuwa kuna jambo linakusumbua stress, hofu kubwa moyoni n.k

Ukipambana na suala linalokupa presha ndipo utatibu presha hiyo. Vinginevyo hata ule mawe. Ndio maana utasikia watu wanakwambia tuliza presha, presha ya nini?

Yaani ili uwe na presha lazima kuna kitu kinaelemea moyo wako.
Azingatie sana
 
Back
Top Bottom