Msaada: Nimepatwa na changamoto kwa "Wife" na huyu dada

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,515
Nimeyumba kidogo kiuchumi toka mwezi wa 1. Kutokana na Corona na sehemu nyingi duniani kuyumba kiuchumi pia.

Binafsi huwa nanunua kila kitu mwisho wa mwezi na kuweka nyumbani, kila kitu kwa maana ya kwamba hata ikitokea mwezi mzima tukaamua kukaa ndani bila kutoka tutaishi vizuri tu. Pia mwisho wa week naenda nunua vegetables like nyanya, vitungu, carrots etc ambavyo haviwezi kaa mwezi hadi mwezi. Pamoja na hayo kila siku naacha Tsh. 7000 nyumbani. Hiyo siulizi watanunulia nini coz kila kitu kipo mafuta, gesi, sukari, mchele n.k

Kutokana na hali ya uchumi kuyumba kiwango cha kucha home kilipungua from 7000 mpaka 5000 na sometimes 4000. But still mahitaji mengine kama kawaida, hapo nami najiwekea mafuta kila week kwenda kazini.

Wife hajawa muungwana. Nampa pesa sometimes anafoka sasa hii ya nini (kwa maana ya kwamba ni ndogo kuacha home). Pamoja na kuwa hata yeye anafanya kazi but akinunua kitu lazima nije kumrudishia pesa. So imefikia hatua nikawa napata mawazo sana, binti mmoja aliona sipo ok huyu ni rafiki toka miaka ya nyuma sana 2014.

Sababu ya kujali na nini akawa karibu nami na mwishowe tukawa wapenzi, kiuhalisia yeye anaonesha kujali sana, atanipa pole, atanisaidia napokwama n.k. nimejaribu kumwambia sipo vizuri kiuchumi ili anikimbie ndio kwanza ananitia moyo.

Hili huwa linanitesa sana, anaonesha kunipenda no matter what na kuniheshimu, nilijaribu kuangalia kuwa maybe mke wangu ana nicheat miaka yote hii sijapata ushahidi wowote, so yupo hivyo tu ni mkaidi na si mtu wa huruma sana. She is cold hearted. Mjeuri sana kwa almost kila mtu hana marafiki wengi na mara nyingi hugombana na rafiki zake coz anajiona ni much better than them.

Sasa napata shida huyu mpango wa kando sometimes ndio nawish angekuwa mke ana sifa zote kwa uzuri wa sura na umbo na very romantic pia, ingawa hana elimu kubwa ana certificate tu. Sasa inafikia hatua nawaza kufanya naye mambo ya maendeleo coz anapokuwa na jambo ananishirikisha nikimshauri anafanya tofauti na wife ni mkaidi mpaka jambo liharibike ndo anakubali alikosea.

Huyu dada nilimshauri aache kazi alipokuwepo afanye biznez flani akaacha kweli na kuanza kwa nguvu hiyo business. Sasa anatengeneza pesa, anajituma sana. Mdada anaondoka saa 11 na kurudi home saa 2 usiku ukimwona huwezi mdhania sababu ya uzuri na mwili wake but si mvivu hata kidogo.

Pia, kwenye mapenzi anajituma sana, anaonekana kabisa ana enjoy mapenzi sana nami popote tuna make love na kufurahi. Wife tukifanya naye akimaliza tu hapo anaanza kunambia nimalize na sometimes ananiacha sijamaliza anaomba alale. Hii nayo ni shida kwangu.

Sasa najikuta kwenye hard time sana maana huyu dada ananipenda na kunisikiliza sana. Nikimwambia jambo analifanyia kazi na si kwa sababu anapata pesa kwangu, No yaani yupo hivyo tu.

Naumia ndugu zanguni nawaza nifanye nini sababu nashindwa kumwacha huyu dada hata kumtafutia sababu ni ngumu. Hajanikosea toka miaka yote namfaham hajawahi nikosea. But naumia pia namsaliti mke wangu. Nipo njia panda sana katika hili nahitaji faraja lakini aliyepaswa kunipa faraja doesnt do that badala yake mtu mwingine kabisa ndio anachukua jukumu hilo.

Ushauri wenu.
 
Mkuu kwakuwa ushaamua kujustify usaliti wako haina noma wewe endelea.

Ila kumbuka kila mtu ana mapungufu yake ni vile tu uwa nikufanya uamuzi wa kuzingatia yaliyo mema zaidi ya yaliyo mabaya. Walau haja kucheat. Kuna mwanamke namfahamu, akiwa na mumewe mahaba kama yote full kumpost insta na macaption matam matam, lakini huku nyuma anatembea na rafiki yangu flani.

Kupanga ni kuchagua naona umekoleana penzi la bi dada lazima kila utakalofanyiwa na mkeo uliweke kwenye kipimo kumlinganisha na huyo bidada.
 
Acha kucheat mkeo na anza kuangalia mazuri ya mkeo, kumbuka machale yake na kihisia haupo nae unasex sababu unatakiwa kutimiza wajibu na si kwa mapenzi. Kinachotekea mkeo anahisi kutengwa kihisia na ndiyo maana anakuwa mkali mkali ..
Huyu mwanadada inabidi ujitahidi uachane nae kama kweli unampenda naamini kamabunampenda utajali hata kesho yake , uzuri huwa unaisha na jua kila siku inayopita kuna kitu kinapungua ..
 
Polygamy si dhambi..
Kaa nao wote wawili au nenda Kwa DC uwe na polygamy ya Siri..mkeo mkaidi asijue..


Mkeo anaweza kuwa pia hajapendwa enough..
Ana ukosefu wa upendo na maalezi na wewe huna mda WA kuwa mume na baba..
Unaaenda nae kizungu ..mambo ya equal partner..

Wanawake wengine wanataka mume uwe baba pia hata kumzaba vibao akikosea
 
Ila hiyo ya kuzaba vibao duh
Polygamy si dhambi..
Kaa nao wote wawili au nenda Kwa DC uwe na polygamy ya Siri..mkeo mkaidi asijue..


Mkeo anaweza kuwa pia hajapendwa enough..
Ana ukosefu wa upendo na maalezi na wewe huna mda WA kuwa mume na baba..
Unaaenda nae kizungu ..mambo ya equal partner..

Wanawake wengine wanataka mume uwe baba pia hata kumzaba vibao akikosea
 
Huyu Mke wako mnawatoto kwenye familia?Umedumu naye muda gani??
Yupi unampenda kweli?? Je dini yako inaruhusu kuoa mke wa pili?

Kunajamaa aljacha mke wake akalogwa mpaka akadead .Mbona wife wako anakuwa mtukutu tabia yake huichunguza kabla unao

Je unaweza kuwahandale wote wawili??
Je huyo mwenye certificate anajua unamke??
Ukiweza owa wote !
Mwambie wife akiendelea hivyo utamwacha .

Kuna Mwalimu alikosana na mke wake Nyumba ikamshinda kabisa akahama akaenda kujenga na kuishi pengine
Chakushangaza yule mwanamke akamtumia Majamba yakamnyonga yeye na kaka yake

You grown up .Enough to think and do it
THINK
T--- is it True
H-- is it Helpful
I --- is it Important
N-- is it Necessary
K-- is it Kind

Fikiria sana sana hata watu wakitoa ushauri hapa
Kazi kwako sasa Mkuu
 
Back
Top Bottom