Msaada: Nimeona wazazi wangu wakifanya mapenzi, je ni mkosi au laana?

bishororo

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
254
358
Ndugu wana JF,

Kama mwezi uliopita nimenda kijijini kumsalimia baba na mama kwa bahati mbaya usiku mmoja hivi nilikuwa natoka nje kukojoa nilikuta mzee na bi mkubwa wakifanya yao sebuleni.

Nikarudi kimya kimya chumbani kwangu wenyewe hawakuniona. Sasa mpaka Leo ile taswira inanisumbua sana nahisi ni laana na mkosi sababu mambo yangu si mazuri toka siku hiyo nimekuwa sijielewi kama chizi.

Naomba msaada, nifanyaje?
 
Aiseee,
16464427_1871489053063402_5198701382277791744_n.jpg
unasingizia ulirudi chumban wakati ulifaidi mechi huku ukiwa refa kisiri siri halafu unakuja lalamika hapa.
 
Pole sana mkuu. Ni kweli jambo kama hilo lazima likusumbue kisaikolojia japo kwa muda. Ukweli ni kwamba hiyo haiwezi kuwa laana wala mkosi iwapo hukukusudia wala hukuwapiga chabo makusudi. Kama uliwapiga chabo hapo hilo ni kosa kubwa na kiukweli ni mkosi. Cha kuzingatia hiyo habari ukae nayo mwenyewe kimya kimya wala usithubutu kumsimulia MTU YEYOTE (humu ni tofauti maana hakuna anayekujua wewe wala hao wazai wako)

Sasa kama unajiona umeshakuwa mtu mzima busara ya ukomavu inatuelekeza kwamba katika mazingira kama hayo ya kushirikiana nyumba ya kulala na wazazi kama hivyo wamelala sebuleni wewe ndani, kama utatakiwa kupita mahala walipopumzika wazazi wako usikurupuke tu kama mtoto mdogo. Lazima utoe alart ya kiutu uzima kama kukohoa, au kujifanya unamkemea paka au panya kwa sauti hata kama unajua hakuna kitu - ili mradi kutoa sauti ya kuwastua kwamba uko macho ili wajiweke sawa ndipo utoke, na siyo kuwatambuka kimya kimya. Maana hata kama hawafanyi mambo ya kikubwa wanaweza wakawa wamelala wamejiachia - unajua usingizi tena, nguo hawana au mmoja akatoa sauti ya kupumua (nadhani unanielewa) - yote hayo ni majanga kwa wewe mtoto kuyashuhudua.

Haya maadili sisi tulikuwa tunafundishwa shule za jandoni. Sasa makabila mengine yasiyokuwa na jando sijui wanapataje maadili haya.
 
Loooh
Bwana usiogope hukufanya makusudi, wao walitakiwa waende chumbani wakijua hawako wenyewe.potezea image inakujia sababu ushajiwekea akilini mwenye kuwa ni mkosi au laana, kumbuka ukiwazacho ndicho kikutokeacho. Kuwa na positive mind na potezea kama hukuona kitu
 
Ndugu wana jf kama mwezi uliopita nmenda kijijini kumsalimia baba na mama kwa bahati mbaya usiku mmja iv nilikuwa natoka nje kukojoa nlikuta mzee na bi mkubwa wakifany yao sebuleni nkarud Kimy Kimy chumban kwang wenywe hawakuniona Sasa mpk Leo Ile taswira inansumbua sana nahis ni laana na mkosi sbbu mambo yng c mazur toka Cku iyo nmekuwa cjielew kama chizi naomba msaada nfanyaje
Pole. Wamezoea kujinafas. Hakikisha unakohoa au una vuta miguu kabla hujatoka. Na mliozoea kuingia vyumba vya wazazi wenu, hata kama ni wazee, bila kugonga muache tabia hiyo.

Hamna laana kama hukukaa kuangalia zaidi.
 
Usijisikie vibaya, hayo mbona ya kawaida tu, vp kama ungemfuma bi mkubwa hapo sebuleni akidet na mwanaume tofauti na baba yako, hapo si ndo ungechanganyikiwa kabisa! Kuwa na amani bwana mdogo, siku nyingine fanya alerts kadhaa ndipo utoke chumbani kwako!
 
Kweli ni laana inakuendesha si unaona hata mdogo wako alikimbia na mchumba wako pamoja na pesa na kadi ya benki
Jipange laana itakutafuna hiyo ubaki kopo
Nenda kawaombe msamaha uwaambie japo hukukusudia
 
Ndugu wana jf kama mwezi uliopita nmenda kijijini kumsalimia baba na mama kwa bahati mbaya usiku mmja iv nilikuwa natoka nje kukojoa nlikuta mzee na bi mkubwa wakifany yao sebuleni nkarud Kimy Kimy chumban kwang wenywe hawakuniona Sasa mpk Leo Ile taswira inansumbua sana nahis ni laana na mkosi sbbu mambo yng c mazur toka Cku iyo nmekuwa cjielew kama chizi naomba msaada nfanyaje
Acha dhana potofu, elimika macho hayana pazia. Mikosi ingekuwa inakuja hivyo nani asingekuwa nayo duniani hapa?
 
aisee mkuu umeona show ya mshua na bi mkubwa.... hahahahhahaaaaa noma sana!! idanganye tu apo akili yako kwamba ulikua unaota au ulichokiona ni kawaida!!! no way..... vipi lile tatizo lako la kutokuridhika ukifanya mapenzi umeshalipatia solution?
 
Usiweke imani yako ktk hilo maana hukukusudia mambo kuwa mabaya kwa msimu huu ni tatizo linalomkabili kila moja so futa hiyo image ktk akili yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom