Smartphone kwa dunia ya sasa ni muhimu sana haina tofauti na computer.Kuikosa kwa kweli ni sawa na kuishi maisha ya ujima.
Inategemea unatumia mtandao wako kwa vitu gani kama ni kwa ajili ya kupiga tu majungu yasiyo na faida haina maana kwako
Kumbuka simu hiyo unaweza ongea na mtu ukiwa unamuona akakuelekeza kitu ukiwa kazini.Simu hii hii unaweza kutuma email ya kikazi.Unaweza hata kuomba kazi online kwa kutumia simu.Unaweza apply chuo ukapata kama alivyofanya binti yangu ukapata.Unaweza ukakata ticket ya ndege ukiwa kijijini kwenu Kwamsisi ukaenda kupanda ndege KIA na ukijipangia siti ya kukaa hapo hapo kwenye ndege,Unaweza lipia bili ya maji kwa simu,kwa kutumia simu yako unaweza ukawa umesahau kitambulisho chako au kadi ya benki ukatumie QR code ukaiona,unaweza save ticket ya ndege ukaiona kwenye simu yako usitembee na makaratasi.
Unaweza kufanya confrence na kikundi kingine hata mambo ya kikazi
kwa kifupi smart ukiitumia vizuri ni shule tosha sana
Kama unaitumia ku bet na kuangalia ni celebrity gani wamemsema au Diamond na msichana wake mpya wameaachana au vipi inakuwa haina faida kabisa ni bora kuacha
by the way mtoa mada una elimu gani kwanza
ungekuwa umefika chuo kikuu usingetoa hii kitu kwenye mkeka hapa