Msaada: Nilifanya nae biashara kaamua kunidhulumu

Llio 002

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,631
2,038
Habari wana JF,

Kuna jamaa nilifanya nae biashara sasa kaamua kunidhulumu na mpaka hivi sasa namtafuta kwenye simu yake muda mwingine hapatikani na hata akipatikana hapokei simu na sijuwi wapi anapokaa na wala sijuwi ofisi yake ipo wapi.

Nilikutana naye kwenye mtandao tu na tukakubaliana tufanye hiyo biashara na nilikuwa namtumia hela through bank account na muda mwingine through tigo pesa lakini mwisho wa picha biashara ile ikafanyika nisivyo taka kwa hiyo nikataka jamaa anilipe nusu ya gharama zangu lakini ndio hivyo sifahamu anapokaa, sijui ofisi yake na wala sijawahi kukutana naye mimi kama mimi ila msimamizi wangu wa kazi anamjua.

Je wanajukwaa nitumie njia gani niweze kumpata huyu mtu? Na je nikitumia namba yake nikienda either TCRA au Tigo Makao Makuu wanaweza kunipa njia ya kumpata kwa kutumia hiyo namba yake?

Na je ni vipi akibadilisha namba ya simu?

Naombeni msaada tafadhali wakuu
 
Niafadhali nionekane mshamba maswala ya kufanya biashara na mtu ambae mmekutana tu kwenye mtandao hiki kitu sifanyi mkuu kama hamkuandikishana ndio imetoka hivyo vinginevyo labda akuonee uluma tu yy mwenyewe
 
Nadhani yupo hapa anafuatilia namna unavyoweka mikakati ya kumpata na yeye anajipanga namna ya kutegua.

Ianike ID yake hapa ili kama kuna wanaomjua watoe msaada pia kwa faida ya wengine kujihadhari nae mkuu
 
Mpigie simu kwa namba ngeni halafu jifanye unahitaji huduma fulani kutoka kwake mvute ili upate more details.au kama kuna tangazo aliliweka mtandaoni anza upya kwa akaunt na jina jingine jifanye wahitaji huduma.
au mtumie mwanamke ajifanyekuwa amemmiss kimapenzi. Yote haya hayahitaji haraka.Ukikurupuka humpati tena kwa njia yoyote ile
 
Niafadhali nionekane mshamba maswala ya kufanya biashara na mtu ambae mmekutana tu kwenye mtandao hiki kitu sifanyi mkuu kama hamkuandikishana ndio imetoka hivyo vinginevyo labda akuonee uluma tu yy mwenyewe
Hatuna mkataba wa kibiashara mimi na yeye ila kuna zile transaction records je haziwezi kusaidia?
 
Hatuna mkataba wa kibiashara mimi na yeye ila kuna zile transaction records je haziwezi kusaidia?
Kwanza pole.

Pili, kama ana nia ya kukudhulumu haziwezi kusaidia kwa sababu anaweza kusema ulikuwa unamtumia pesa kweli ila alikuwa anakudai so ulikuwa unalipa deni
 
Kwanza pole.

Pili, kama ana nia ya kukudhulumu haziwezi kusaidia kwa sababu anaweza kusema ulikuwa unamtumia pesa kweli ila alikuwa anakudai so ulikuwa unalipa deni
Kweli si mchezo aiseee...sasa nitumie njia gani ili nimpate huyu mtu hebu jaribu kunisaidia hapo mkuu
 
Police sasa hivi wapo busy na watumiaji wa bangi hawawezi kukusaidia, nitafute ntakupa mtu atakusaidia ila utamlipa
 
Niafadhali nionekane mshamba maswala ya kufanya biashara na mtu ambae mmekutana tu kwenye mtandao hiki kitu sifanyi mkuu kama hamkuandikishana ndio imetoka hivyo vinginevyo labda akuonee uluma tu yy mwenyewe
huruma.
 
cha msingi ni kutulia tu! jipange upya ufanye biashara yako wewe mwenyewe hapo hakuna tena jipya umejifunza kitu
 
Hibi mnapata wapi ujasiri wa kumtumia mtu pesa ambaye humjui A wala Z? eti mnafanya biashara!!!

Hiyo ni hatua mojawapo ya kuingia Ukubwani.

Samehe ila usisahau, ukisahau utadhulumiwa tena.
 
Back
Top Bottom