Msaada, nikienda Mahakamani naweza sikilizwa?

mtanzania10

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
271
81
Mimi ni muajiriwa Serikalini. Nilikopa kwa watu wanaotoa riba alafu yeye anabaki na kadi yako ya benki mshahara ukiingia anachukua.

Tulienda nao vizuri baadaye Mambo yaka ingiliana uwezekano wa kuwalipa ukawa haupo nikaanza kuwapiga chenga mshahara ukiingia Mimi natoa kwa NMB Mobile. Jamaa wakawa wanakuja kituo cha kazi nawakwepa kiukweli niliwazungusha sana lengo langu nilikuwa nataka jamaa waende mahakamani wanifungulie kesi lakini jamaa hawakwenda.

Hatimayee tukaonana baada ya kuona ni kero sitaki kusumbuliwa nikawafata tukaanza kulipana tena. Sasa tatizo lililopoo jamaa wanachukua pesa yote. Shida zikaongezeka nikawakwepa tena sasa nina miezi mitatu sijawalipa.

Nilichokuwa nahitaji ni Mimi mwenye niende mahakamani nieleze na niombe niwe namlipa kidogo kidogo hadi deni litakapo isha na kadi yangu anipe yani niwe nachukua laki moja na hiyo inayobaki awe anachukua yeye hadi deni litakapo isha.

Sasa nawauliza hapo nikienda mahakani naweza sikilizwa?
 
Tulienda nao vizuri baadaye Mambo yaka ingiliana uwezeka no wa kuwalipa ukawa haupo nikaanza kuwapiga chenga mshahara ukiingia Mimi natoa kwa nmb mobile.
Hapo umekwenda kinyume na makubaliano yenu kuhusu mahakama kukusikiliza itakusikiliza ila kushinda kesi inategemea na maelezo ya pande mbili. Lakini kisheria hao jamaa hawawezi kuchukuwa kadi ya benki wala hela yako yote manake na wewe lazima upate hela ili uishi.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Lengo ni kuwalipa kidogo sio kuacha kuwalipa na nikae huru bila kusumbuliwa
Hapo umekwenda kinyume na makubaliano yenu kuhusu mahakama kukusikiliza itakusikiliza ila kushinda kesi inategemea na maelezo ya pande mbili. Lakini kisheria hao jamaa hawawezi kuchukuwa kadi ya benki wala hela yako yote manake na wewe lazima upate hela ili uishi.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mkataba wenu ndo utakuweka huru uwez kopa alafu ukwepe kulipa deni hata kama mambo yako si mazuri mkuu

Kama makubaliano ni kuchukua mshahara wotee sheria itakulinda lakini deni lazimaaa ulipe

#Staysafe
 
Mkataba wenu ndo utakuweka huru uwez kopa alafu ukwepe kulipa deni hata kama mambo yako si mazuri mkuu

Kama makubaliano ni kuchukua mshahara wotee sheria itakulinda lakini deni lazimaaa ulipe

#Staysafe
Mimi lengo ni kulipa deni ila na Mimi nibakiwe na laki ili niweze kuishi
 
Kaka kama ulikopa na mliandikiana mkataba lazima ulipe kadiri ya makubaliano.Mahakamani watakachofanya watasikiliza pande zote na kuamua kadiri ya uwezo wa wewe kulipa.Ila pia jamaa hao kama wana kampuni halali na wanalipa kodi serikalini kuna uwezekano ukaamriwa ulipe kadiri ya mkataba wenu.

Pili, kitendo cha kuwakimbia umeonyesha wewe ni tapeli au si mwaminifu, hivyo basi ili kuepuka kero nakushauri mkae chini mmalizane.Mahakamani utapoteza muda ndugu halafu jamaa wakihonga kule itakula kwako tu.Inaonekana wana nguvu ya pesa.Siku nyingine epukana na madeni yasiyokuwa na tija.

Inaonekana ulikopa kwa ajili ya kuspend kununua vitu ambavyo ni liability kwako na sio kuinvest kwenye asset au vitu vya kuzalisha pesa na kama uliinvest kwenye mradi wa kuleta pesa basi ulikosea kusimamia kwa sababu hiyo hela ilipaswa izalishe ikusaidie kulipa deni.
 
1. Dawa ya deni ni kulipa.

2. Makubaliano yenu ni halali isipokuwa namna ya kulipana (kuchukua kadi ya benki n.k) sio halali, kwa sababu;

-Kadi ya benki ni kwa ajili ya mwenye akaunti, benki kwa kukupa ile kadi na wewe kuweka namba za siri, inatambua kuwa ile kadi ni kwa ajiki ya matumizi yako na si ya mtu mwingine.

-wewe kuikabidhi kadi kwa benki, ni uvunjifu wa masharti ya kimkataba baina yako na benki(benki hawamtambui aliyekukopesha kama mfaidika wa akaunti yako).

3. Mkataba ulioingia nao kwa misingi ya wao kushikikia kadi yako ya benki ni batili kwenye kipengele cha kulipana kwa njia ya wao kuingia katika akaunti yako na kuchukua pesa zote kama vile wao ni wewe.

4. Kwa sababu wewe ndiye mwenye mahusiano ya kimkataba na benki, sio wao; unaweza kuielekeza benki kusimamisha ufanyaji kazi wa kadi hako, halafu upange na wadai wako namna nyingine ya kulipana. (KIMSINGI WALIPE MMALIZANE)
 
Huo mfumo wa ukopeshaji sio rasmi kwanza huyo uliemkopa awezi kwenda fungua mashataka. Ila kama wew unaend fungua mashataka ndio unahalisha shataka lako kuw ndani kisheria.

Chakufanya nenda Bank kaombe kadi mpya Toa mshahara wako na kiasi unachojisikia kuwalpa wapelekee mkononi au warushie kwenye simu.

NB: kutumia kadi ya Bank ya mwenzako ni kosa kisheria so awawez kwenda ata siku moja na wew usijipeleke lipa unavyotaka
Hao jamaa japo wanatusaidia ila wa liba kubwaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka kama ulikopa na mliandikiana mkataba lazima ulipe kadiri ya makubaliano.Mahakamani watakachofanya watasikiliza pande zote na kuamua kadiri ya uwezo wa wewe kulipa.Ila pia jamaa hao kama wana kampuni halali na wanalipa kodi serikalini kuna uwezekano ukaamriwa ulipe kadiri ya mkataba wenu...
Mchezo huu wanao walimu, anaenda kukopa kwa wakopaji wa vichochoroni watozao riba kubwa na kuacha ATM card yake na password zake. Na wengi wao hukopa kwenda kunywa pombe na kununua vitu ambavyo ni liabilities.

Mtoa mada bila Shaka ana mikopo NMB, maboto, na mataasisi mengine kibao ya ovyo ovyo.
 
Thus means unataka kuvunja makubaliano ya mkopo na namna ya kulipa. Km mlikubaliana busara itumike nenda tu waelekeze. Mahakamani utafeli koz mlishakubaliana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom