Msaada: Nifanye nini elimu niliyoipata inateketea huku naiona?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,810
Mimi ni Kijana mwenye umri wa miaka 28 hapa tangu nimalize chuo kikuu miaka 4 iliyopita sijafanikiaa kupata ajira na nimeshidwa kujiajiri kutokana na kukosa mtaji wa kibiashara......

Kinachoniuma zaidi KATIKA elimu niliyoipata kila nikikumbuka .....

1.kipindi nasoma tuition hela niliyokuwa ninapewa na mzazi kwa ajiri ya tuition.

2.nikumbuka kipindi nipo secondary hadi Chuo nilivikuwa nalipa hela ndogo ndogo za michango ya hapa na palee.

3.nikikumbuka nilivyokuwa nagombania darasani mchikichini

4.nikikumbuka nilivyokuwa naongoza darasani na kupewa vizawadi vya mwanafunzi bora.

5.kila nikikumbuka jinsi mzazi wangu akiangaika kuitafuta pesa kwa ajili ya Mimi kuweza kusoma.

6.nikikumbuka zile nauli na hela ya shule toka kwa mzazi .

7.nikikumbuka nilivyokuwa nakesha usiku kupiga msuli hadi asubuhii tangia o level hadi Chuo

Leo namshukuru mungu nimemaliza hadi chuo lakini kazi zimekuwa ngumu kupatikana.

Kuna kipindi niliwahi kuwaza kujiua maana roho inaniumaa . .....

Tafadhali naombeni ushauli nifanye nini najiona nipo kipindi kigumu sana
 
Pole. ila sio lazima uanze na mtaji wa mamilioni,,unaweza kuanza hata na mtaji wa elfu 50,au elfu 30, na usione aibu kufanya biasha yoyote ile kisa unaelimu.hutoweza fanikiwa.ukiwa na elimu siku hizi ni kama umeenda kutoa ujinga tu. pambana kijana
 
Pole Mkuu.zamu yako ikifika Mungu akiiamua ata awe nani utapata riziki yako.everything happen for a reason.Nikumshukuru Mungu kwa kukupa uhai.wapo wengi pia wenye shida zaidi yako wanatamani pia walau wangekua wazima kama wewe .ila walemavu au wapo mahospitalini
 
1. Umesoma kozi gani?
2.Je una wazo lolote la biashara? Na unahisi itahitaji mtaji kiasi gani ili kuanza?
3. Umewahi kufikiria kufanya kazi kwa kujitolea? Na je uko tayari?
4. Umewahi kuwaza kufundisha, esp masomo uliyosomea kwa ngazi ya sekondari?
 
Haya maswali yajibu aisee hata kama ulisoma sosholoji wewe tuambie ukweli
 
Ukitaka kufanikiwa idharau aibu! Sidhani kama mtu mzima kama wewe unakosa kabisa hata mtaji wa 50,000/= wa kuanzia japo biashara ndogo. Tatizo lenu vijana wa sasa mnaendekeza ubishoo!
 
Pole Mkuu.zamu yako ikifika Mungu akiiamua ata awe nani utapata riziki yako.everything happen for a reason.Nikumshukuru Mungu kwa kukupa uhai.wapo wengi pia wenye shida zaidi yako wanatamani pia walau wangekua wazima kama wewe .ila walemavu au wapo mahospitalini
Usimlemaze mkuu,
Apige kazi aache ubishoo wa kujifanya msomi,usomi bongo? Abebe zege,awe kondakta n.k akipata mtaji hata wa 100,000/= auze mkaa maisha yasonge!
 
1. Umesoma kozi gani?
2.Je una wazo lolote la biashara? Na unahisi itahitaji mtaji kiasi gani ili kuanza?
3. Umewahi kufikiria kufanya kazi kwa kujitolea? Na je uko tayari?
4. Umewahi kuwaza kufundisha, esp masomo uliyosomea kwa ngazi ya sekondari?
Mimi nimesomea maswala ya social work .

Napenda sana kufanya biashara na huwa Nina wazo sana LA kufanya hivo ila tatizo mtaji .

Kujitolea nimeshawahi kujitolea sehemu tofauti tofauti .

Kufundisha kwa kweli hapo badoo
 
Pole. ila sio lazima uanze na mtaji wa mamilioni,,unaweza kuanza hata na mtaji wa elfu 50,au elfu 30, na usione aibu kufanya biasha yoyote ile kisa unaelimu.hutoweza fanikiwa.ukiwa na elimu siku hizi ni kama umeenda kutoa ujinga tu. pambana kijana
Nashukuru kwa ushauli wako niliupata toka kwako
 
Pole Mkuu.zamu yako ikifika Mungu akiiamua ata awe nani utapata riziki yako.everything happen for a reason.Nikumshukuru Mungu kwa kukupa uhai.wapo wengi pia wenye shida zaidi yako wanatamani pia walau wangekua wazima kama wewe .ila walemavu au wapo mahospitalini
Asante sana Mkuu kwa ushauli ulionipatia
 
Kijana wa miaka 28 unakata tamaa mapema hivyo na kutaka kujiua?? Embu muogope Mungu basi..
 
Back
Top Bottom