Msaada: Neno 'background' kwa kiswahili

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,204
5,704
Naomba tafsiri ya neno hilo kwa kiswahili likitumika katika muktadha wa uandishi wa taarifa( report) au kitabu pale mwanzoni.

Kwa mf

Introduction
Background
Preface
 
Dibaji = Preface/ Foreword ?? Ingawa Preface inaandikwa na author na foreword na mtu mwingine. Otherwise similar.
Introduction = Utangulizi
Background = ???
 
He he he mkuu kiswahili kinachangamoto ya maneno mepesi sana.
 
Kuna mtu kaniambia Background ni Usuli. (Disclaimer)

Tuangalie Kamusi za TUKI (leo:TATAKI, yaani Taasisi ya Taaluma za Kiswahili , Chuo Kikuu Dar ) :
1. English-Swahili
"(back-)
~ground n 1 usuli. 2 mahali pa nyuma (sehemu ya sanamu, picha n.k.). 3 mahali pa kufichia. 4 muziki wa chinichini."

Kuhusu "mahali pa nyuma" nina wasiwasi nisingeitumia kwa sehemu ya picha, sidhani ni sahihi hapo. Hapo ningetumia "sehemu ya nyuma" au "eneo la nyuma".

2. Kamusi ya Kiswahili Sanifu
"usuli nm 1. asili. 2 taarifa ambayo ni muhimu katika kuelewa tatizo au hali"
 
Kw

Kwahiyo neno USULI ni sahihi
 
Kwa maelezo yaliyotangulia nami naona USULI ni sahihi.
Ila tu inategemea unamaanisha nini kwa "background". Kwa maana ya kutaja yale nyuma ya mawazo au mafundisho - usuli inaweza kuwa sawa. (Usuli ya hofu yake ni maarifa mabaya aliyokuwa nayo zamani)

Lakini kama ni mahali au eneo - itakuwa ni mandharinyuma. (=nyuma ya mandhari). Kwa hiyo ukipiga picha ya mtu yale yaliyoonekana nyuma yake ni mandharinyuma, si usuli.
 
Back
Top Bottom