Msaada ndugu zangu.

Msaada ndugu zangu.

Mothersuperior

New Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
1
Reaction score
4
Habarini?
Mi ni mwanajf wa kuperuzi kama guest. Lakini leo nimepatwa na nimelazimika kupata ac ili mnisaidie kwa ushauri.
Ipo hivi, mimi nilikua na mpenzi ambaye huu ni mwaka wa tatu sasa. Miaka miwili nyuma ilikuwa ni furaha na pia alikuwa akitaka hata aje kujitambulisha rasmi. Nyumbani walimjua na aliweza kuja muda wowote hata kama sipo nami pia nilijulikana kwao hata kama hayupo niliweza kwenda. Kiufupi kila mmoja alikuwa free na comfortable.
Shida imeanza mwaka wa tatu wa mapenzi yetu. Mwenzangu mapenzi yalishuka. Kupiga simu ilikuwa shida. Nikimpigia yu busy. Kila siku alikua ananiletea visa. Hata pasipo na kosa ye alilitafuta kosa lilipo akalipachika. Nakumbuka kipindi hiko nililia sana. Nilisali sana. Lakini mambo hayakubadilika. Mwisho wa siku mwenzangu akaniambia kuwa amepata replacement yangu hivyo hanihitaji katika maisha yake.
Tatizo linalojitokeza ni moja. Kiukweli mi nampenda sana. Ye ni kama ndugu yangu mbali na mpenzi tulikuwa kama marafiki na ndugu. Shida zake zangu na zangu ni zake. Tumeshajaribu kufanya projects mbalimbali.
Baada ya vituko vyote alivyonifanyia, nikamwambia mwenzangu yeye ni kama ndugu yangu. Maswala ya projects zetu zisikatike sababu ya mapenzi. Mi nimeshachoka kuhangaikia mapenzi hivyo tuendeleze kazi za kimaendeleo tu. Hata akitaka kuoa mi roho yangu ni nyeupe kabisa. Taratibu nitamuona ni mtu wa kawaida. Ila shida mwenzangu aliongea na baadhi ya watu kuwa hata iweje hawezi kuniacha. Ataenda kote lakini atarudi tu kwangu. Na pia mimi ninamtreat kama mtu wa kawaida kwa sasa lakini yeye bado ananitreat kama mpenzi. Hataki kabisa tushirikiane kimaendeleo zaidi. Kila anapojaribu kunisogelea bado anataka tuendeleze mapenzi. Anajilazimisha kujiweka mbali na mimi kwa nguvu sana jambo ambalo linamuathiri. Baada ya muda kidogo ananiomba msamaha sana
Ndugu zangu nipeni ushauri. Haiwezekani kabisa mimi kuwa na huyu mtu kwa ajili ya kazi tu?
Naombeni mnishauri ndugu zangu ili nipate kurekebisha hili tatizo. Sitaki chuki iwepo kati yetu. Kama upendo umeisha basi ibaki tu maisha ya kawaida maana kwao na kwetu wamekuwa family friend sasa. Lolote likitokea tunajumuika sote.
 
Wazo lako la kwanza ndilo la kulifanyia kazi, maana miruzi mingi humpoteza mbwa.
 
Mbona hueleweki mara alisema kapata mwingine mara unampenda sana mara kasema hawezi kukuacha sijui anaomba msamaha


Sijui hata unataka ushauri gani
 
Pole sana, jaribu kutulia kwanza na kutafakari...usisumbuane nae sana ukiona hana ramani mpotezee tu usonge mbele kuliko kujitoa kwa mtu asiye na muda na wewe
 
mi ni kama sijaelewa vizuri, ngoja nitarudi
 
Pole, huo urafiki unaong'ang'ania utakutesa sana, gawaneni ivo vitu kila mtu aangalie njia yake fullstop, yaani uchumba wa miaka mitatu tu unaogopa kuachana, kuna watu walioana kwa ndoa na waliishi miaka 16 na walizaa watoto 8 na waliachana na kila mmoja kaendelea na yake Hlf wewe unalilia mchumba asekutaka,
Halafu unasema hata akioa huna shida hahahaa naona unautafuta umchepuko wa kudumu wanawake tukoje jamani huyo mtu anakupenda kwa vile unajua kutafuta pesa tu si vinginevyo
 
Mahusiano huwa yanakuja yenyewe, hayalazimishwi, haijalishi ni ya aina gani. Mmejaribu na mmeshindwa kuwa kwenye ukurasa mmoja, kila mtu achukue ustaarabu wake.
 
Mkuu mbona hueleweki mara unampenda sana.

Sasa amerudi na kuomba msamaha wewe umejibu nini??

Hakuna urafiki wa simba na swala.

Mara nyingi urafiki huo uishia kugegedana tu japo wachache wanashinda ya dunia.
 
Wewe endelea na msimamo wako wa kazi kazi

Ila ukaribu na mtu uliyewahi ku-date nae kwangu mimi naona sio sawa...kuna ile moment of weakness mnaweza kujikuta mnakumbushia
 
AMEPATA REPLACEMENT LAKN BDO UNASEMA HAWEZ KUKUACHA? NA HATA KUSHRIKIANA KWENYE MAENDELEO HATAKI? KIUFUP WEWE ANAKUFANYA WA AKIBA. YAN AENDELEE KULA PAPUCH TU HUKU YAKE YAKINYOOKA YAKO YANADODA.

MY SISTER ACHANA NA HUYO MWANAUME IKIWEZEKANA MBLOCK ANAKUPOTEZEA MDA NA ATAKUHARIBIA MAISHA.
 
Mbona hueleweki mara alisema kapata mwingine mara unampenda sana mara kasema hawezi kukuacha sijui anaomba msamaha


Sijui hata unataka ushauri gani

Hawa watakuwa bado wanamegana Ila wote wajanja wajanja
 
Habarini?
Mi ni mwanajf wa kuperuzi kama guest. Lakini leo nimepatwa na nimelazimika kupata ac ili mnisaidie kwa ushauri.
Ipo hivi, mimi nilikua na mpenzi ambaye huu ni mwaka wa tatu sasa. Miaka miwili nyuma ilikuwa ni furaha na pia alikuwa akitaka hata aje kujitambulisha rasmi. Nyumbani walimjua na aliweza kuja muda wowote hata kama sipo nami pia nilijulikana kwao hata kama hayupo niliweza kwenda. Kiufupi kila mmoja alikuwa free na comfortable.
Shida imeanza mwaka wa tatu wa mapenzi yetu. Mwenzangu mapenzi yalishuka. Kupiga simu ilikuwa shida. Nikimpigia yu busy. Kila siku alikua ananiletea visa. Hata pasipo na kosa ye alilitafuta kosa lilipo akalipachika. Nakumbuka kipindi hiko nililia sana. Nilisali sana. Lakini mambo hayakubadilika. Mwisho wa siku mwenzangu akaniambia kuwa amepata replacement yangu hivyo hanihitaji katika maisha yake.
Tatizo linalojitokeza ni moja. Kiukweli mi nampenda sana. Ye ni kama ndugu yangu mbali na mpenzi tulikuwa kama marafiki na ndugu. Shida zake zangu na zangu ni zake. Tumeshajaribu kufanya projects mbalimbali.
Baada ya vituko vyote alivyonifanyia, nikamwambia mwenzangu yeye ni kama ndugu yangu. Maswala ya projects zetu zisikatike sababu ya mapenzi. Mi nimeshachoka kuhangaikia mapenzi hivyo tuendeleze kazi za kimaendeleo tu. Hata akitaka kuoa mi roho yangu ni nyeupe kabisa. Taratibu nitamuona ni mtu wa kawaida. Ila shida mwenzangu aliongea na baadhi ya watu kuwa hata iweje hawezi kuniacha. Ataenda kote lakini atarudi tu kwangu. Na pia mimi ninamtreat kama mtu wa kawaida kwa sasa lakini yeye bado ananitreat kama mpenzi. Hataki kabisa tushirikiane kimaendeleo zaidi. Kila anapojaribu kunisogelea bado anataka tuendeleze mapenzi. Anajilazimisha kujiweka mbali na mimi kwa nguvu sana jambo ambalo linamuathiri. Baada ya muda kidogo ananiomba msamaha sana
Ndugu zangu nipeni ushauri. Haiwezekani kabisa mimi kuwa na huyu mtu kwa ajili ya kazi tu?
Naombeni mnishauri ndugu zangu ili nipate kurekebisha hili tatizo. Sitaki chuki iwepo kati yetu. Kama upendo umeisha basi ibaki tu maisha ya kawaida maana kwao na kwetu wamekuwa family friend sasa. Lolote likitokea tunajumuika sote.
Muogope mtu mwenye sura mbili..huyo hana msimamo na hajui mwelekeo wake ni upi..kuwa care maana atakuja kukuumiza zaidi baadae..ataombaje msamaha then baada ya muda mfupi arudia kosa hilo hilo..jiamini..hata kama ni projects kila mmoja ajue maisha yake..uwe na msimamo asije akahisi wajipendekeza kwake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom