Msaada ndugu zangu wa JF.

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Kama kuna mtu hapa anaejua gharama za kusafirisha mwili wa marehemu kutoka London mpaka Dar aniambie,kuna mdogo wangu wa kike aliolewa na mzungu kafariki huko sasa jamaa kautelekeza mwili kwa coroner nahitaji kuurudisha hapa kwa mazishi sijui itanigharimu kiasi gani.Ntashukuru mkinipa hata estimate.
 
pole sana ndugu yetu. hauhitaji msaada wa kifedha? halafu jaribu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania.
 
Pole sana Uporoto....Mungu akupe nguvu....waweza uliza kwenye makampuni ya ndege na ubalozi wa Tanzania wanaweza kukupa msaada katika hili.....kwani hakuwa na marafiki? wangewezakufanikisha hili,kama wanahitaji hela unawapa,mwili unaadaliwa wanauweka kwa ndege unaletwa....so sad,pole!
 
Pole sana mkuu. Japo ni gharama lakini cheki na huyo coroner kujua gharama za kumsafirisha kuna Watz wengi UK wana jumuia ambazo zimeshafanya jambo kama hili,hata humu JF wapo wanajua wanaweza kuassist
 
pole sana ndugu yetu. hauhitaji msaada wa kifedha? halafu jaribu kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania.
Asante fedha sio tatizo na kuna mtu nikimtumia atafanikisha huko london.

Pole sana Uporoto....Mungu akupe nguvu....waweza uliza kwenye makampuni ya ndege na ubalozi wa Tanzania wanaweza kukupa msaada katika hili.....kwani hakuwa na marafiki? wangewezakufanikisha hili,kama wanahitaji hela unawapa,mwili unaadaliwa wanauweka kwa ndege unaletwa....so sad,pole!
Huwezi amini nimeongea na British airways wakanihamishia Cargo and would you believe anaehusika hajui itagharimu kiasi gani ?
 
Pole sana, wasiliana na ubalozi, wanaweza kushughulikia kuusafirisha hadi JKA na baada ya hapo ww utaingia gharama za kuupeleka kwenu kwa taratibu nyingine. ukiwa hapa bongo, unaweza kufika wizara ya mabo ya nje inapakana na hotel ya kilimanjaro kempsink ulizia idara ya ulaya wanaweza kuwa na msaada mkubwa
 
Pole sana ndugu yangu. Nakuombea Mungu akupe nguvu na Ujasiri ktk kipindi hiki kigumu. Akutangulie kwa chochote utakachofanya. All the best mpendwa.
 
Huwezi amini nimeongea na British airways wakanihamishia Cargo and would you believe anaehusika hajui itagharimu kiasi gani ?

Pole sana Mkuu, huko British airways cargo pia hukusaidiwa? Jaribu kuwasiliana na ubalozi, naimani utasaidiwa. Pole sana.
 
Zika huko huko hizo gharama zingine za nini? mkimalizana na crematorian chukua majivu njoo nayo bongo
 
Asanteni kwa pole zenu wandugu mwili uko kwenye friji wiki ya pili nahitaji kujua nitume kiasi gani upakiwe kwenye ndege pronto.
 
Poleni sana.
Nafikiri ukiwasiliana na ubalozi wa bongo watakusaidia kwa hilo.
Huyo mzungu nae kumtelekeza dada yetu hapa inakuwaje? Roho mbaya haina kabila wala rangi!
Poleni sana mkuu
 
Pole sana dearest......
Kama wapo ambao wamewahi kusafirisha ndo watakaokujulisha vizuri!!!

Baba mchungaji watu wengine wanapenda ndugu zao wazikwe nyumbani!!!
 
Dah! Pole sana Ndugu

Wasiliana na High Commission watakusaidia esp kwenye logistics - maana kama ametelekezwa siyo rahisi pia kuutoa kwa urahisi - kuna utaratibu wake hapo..
 
Poleni sana.
Nafikiri ukiwasiliana na ubalozi wa bongo watakusaidia kwa hilo.
Huyo mzungu nae kumtelekeza dada yetu hapa inakuwaje? Roho mbaya haina kabila wala rangi!
Poleni sana mkuu
wazungu wana roho mbaya sana ,mimi nimeishi sana nchi za europe na sasa hivi naandika kitabu changu na baadi ya nakala nitaiweka hapa JF ,
kama ulikuwa hujui ni kuwa mzungu yeye anakuwa na interest na wewe kama anajua kuwa una faida kwake lakini ukishakuwa huna faida kwake basi , mzungu hana time na wewe.and in nature mzungu hampendi mwafrika im sure no one will say that iam a lie
 
Poleni sana.
Nafikiri ukiwasiliana na ubalozi wa bongo watakusaidia kwa hilo.
Huyo mzungu nae kumtelekeza dada yetu hapa inakuwaje? Roho mbaya haina kabila wala rangi!
Poleni sana mkuu
hili liwe fundisho kwa kinadada zetu wanaowapapatikia wazungu.
 
Huwezi amini nimeongea na British airways wakanihamishia Cargo and would you believe anaehusika hajui itagharimu kiasi gani ?

Nenda kwenye ofisi zao kabisa,za British Airways na Emirates......zaidi nenda ubalozini hapa Tanzania.....watakushauri na kukusaidia Uporoto.

Mumewe huwezi wasiliana nae? what kind of a husband is he ashindwe hata kuwapa ushirikiano kwenye hili jamani??? pls,nenda ubalozi,wape details za mume watamuweka sawa tu na atashirikiana nao kuweza kuutunza na kuusafirisha mwili.....!
 
dada yangu huwezi jua , inawezekana ni hawa wanaume wa u turn.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom