Je unapajua RITA?Fafanua mkuu
Ukizipata ndio umroge?Nataka hela zangu kwanza ..
Asante kwa ufafanuzi ndugu Petro,nimefaidika na mimi kidogo japo sina tatizo kama hilo naimani nitaweza kusaidia watu wenye uhitaji kama wa microsoft.Samahani ningependa kuuliza kwa niaba ya Microsoft ili tuzidi kupata ilmu,Je hakimu hawezi kushirikiana na huyo hakimu tajwa kwa vile wanajuana kumkandamiza mlalamikaji?Je Huyo hakimu hawezi kufunguliwa mashataka kwa ubadhirifu wa fedha za mlalamikaji kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu?Je hakimu hawezi kufunguliwa mashtaka kwa kushtakiwa na mlalamikaji akawa na mwanasheria wa kusimamia swala hili?Mkuu Microsoft , kwanza niwie radhi kwa kuchelewa kuitikia wito wako kwakuwa jana nilitingwa mno na majukumu ya kulijenga taifa letu. Pili, nataka kujua kama wewe ndiwe mtoto pekee wa marehemu uliyemzungumzia. Tatu, wakati wa uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi (naamini uteuzi ulifanyika rasmi Mahakamani), ulikuwa na umri gani? Kwanini hukuteuliwa wewe kama ni mtoto pekee wa marehemu?
Nne, Mkuu Microsoft , kisheria, Msimamizi wa Mirathi si mtu anayepaswa na mwenye haki ya kufaidi mirathi kuliko yeyote awaye. Yeye hupewa majukumu ya kisheria na Mahakama inayomteua kusimamia mirathi kwa faida ya warithi. Wakati mwingine, Msimamizi wa Mirathi naye huwa mmoja wa warithi (akitajwa hivyo na Hukumu ya Mirathi ya Mahakama). Kikubwa ni kuwa Msimamizi wa Mirathi ni msimamizi tu, si aliyerithishwa pekee na kupewa haki ya kufaidi mirathi kuliko wengine.
Kimahakama, jalada la mirathi huwa halifungwi. Yaani, jalada la mirathi halifiki mwisho kirahisi. Sababu kubwa ni pamoja na kurekebisha kasoro zozote zinazoweza kujitokeza katika mirathi husika. Kasoro hizo ni pamoja na zinazomhusu Msimamizi wa Mirathi. Kimsingi, Msimamizi wa Mirathi aweza kubadilishwa au kuondolewa. Ni pale anapofariki au kuugua kwa muda mrefu au hata anapokiuka majukumu yake. Ndiyo kusema, Msimamizi wa Mirathi si mtu wa kudumu katika kuteuliwa kwake.
Kama yeyote mwenye maslahi kwenye mirathi husika ana malalamiko yoyote dhidi ya Msimamizi wa Mirathi, anapaswa kuyawasilisha malalamiko hayo Mahakama ile ile iliyomteua Msimamizi huyo. Labda kama Mahakama ile husika itakataa kuyapokea na kuyasikiliza malalamiko hayo. Mlalamikaji, katika muktadha wako hapa, atapaswa kuthibitisha kuwa Msimamizi wa Mirathi amekiuka au anakiuka wajibu wake wa kisheria wa kusimamia mirathi husika ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume na maagizo ya kimahakama wakati wa uteuzi wake.
Mkuu, si jambo jema kuwa na wasiwasi na Mahakama tangu mwanzo. Pili, masuala ya mirathi yanamalizwa katika taratibu za kimirathi, si kama jinai. Msimamizi wa Mirathi akiondolewa rasmi, masuala ya kijinai yanaweza kuripotiwa na hatua stahiki kuchukuliwa. Katika kesi za jinai hapa Tanzania, Jamhuri ndiye mwendeshaji kupitia Waendesha Mashtaka wa Serikali. Bado hakuna mazoea ya Mwendesha Mashtaka binafsi.Asante kwa ufafanuzi ndugu Petro,nimefaidika na mimi kidogo japo sina tatizo kama hilo naimani nitaweza kusaidia watu wenye uhitaji kama wa microsoft.Samahani ningependa kuuliza kwa niaba ya Microsoft ili tuzidi kupata ilmu,Je hakimu hawezi kushirikiana na huyo hakimu tajwa kwa vile wanajuana kumkandamiza mlalamikaji?Je Huyo hakimu hawezi kufunguliwa mashataka kwa ubadhirifu wa fedha za mlalamikaji kwa kosa la kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu?Je hakimu hawezi kufunguliwa mashtaka kwa kushtakiwa na mlalamikaji akawa na mwanasheria wa kusimamia swala hili?
Natanguliza shukurani kwa majibu yako mazuri.
Ameshafafanua kwamba taarifa za benki zinaonyesha tayari jamaa keshachota kiasi cha pesa milioni kumi.Mkuu Microsoft , kwanza niwie radhi kwa kuchelewa kuitikia wito wako kwakuwa jana nilitingwa mno na majukumu ya kulijenga taifa letu. Pili, nataka kujua kama wewe ndiwe mtoto pekee wa marehemu uliyemzungumzia. Tatu, wakati wa uteuzi wa Msimamizi wa Mirathi (naamini uteuzi ulifanyika rasmi Mahakamani), ulikuwa na umri gani? Kwanini hukuteuliwa wewe kama ni mtoto pekee wa marehemu?