Msaada: Naweza kufika Namibia kwa basi?

Msaada: Naweza kufika Namibia kwa basi?

Nenda Chato hizo fursa unazozifuata Namibia utazipata pale.

Ukiondokana na fikra hizi.....utapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako zaidi ya hata hapo ulipo

Nguvu kubwa ,muda na akili unavyotumia kwenye siasa ungevielekeza kwenye maisha yako ungekuwa umefanya maamuzi yenye busara Na manufaa sana

NB:
SI KWA UBAYA.....
 
asante sn mkuu nategemea january kuanza safari nitaleta mrejesho
mkuu mimi nawaza kwenda sychellies au mauritius ni kila ulaia wa mauritius nadondoka monaco kama naenda zenji... na monaco to ufaransa ni kugusa hivyo... nategemea kutafuta uraia tofauti na huu... maana hapa kwetu... tia maji tia maji hali si shwari... tuna umizana kwa makusudi nchi yetu sote lakini wengine wanatutumia kama matambala ya deki,,,, wana tuona kama wajinga .... ina kera sana....

tuta rudi kama wawekezaji.... wakina payet, nani na wengine wametokea tulipo wameenda walipo... na sisi tusonge mbele ndio maendeleo tusibaki hapa hapa na kulia lia tu wakati fursa si lazima hapa nchini tu
 
Ukiondokana na fikra hizi.....utapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako zaidi ya hata hapo ulipo

Nguvu kubwa ,muda na akili unavyotumia kwenye siasa ungevielekeza kwenye maisha yako ungekuwa umefanya maamuzi yenye busara Na manufaa sana

NB:
SI KWA UBAYA.....
hakika....
 
Safari njema mkuu.

Kufika kule itakubidi upitie Lusaka-Zambia au Lilongwe-Malawi kisha ndo upate basi za kukupeleka Namibia.
Kuhusu maeneo ya kufikia, unaweza kufikia Windhoek mji mkuu wao au ukaenda Swakopmund na Wavis miji iliyopembeni magharibi mwa nchi ikipakana na bahari ya Atlantic.

Kuhusu kazi za ovyo ovyo sijajua utafanya vipi, labda kuulizia kazi za supermarkets, vibarua vya ujenzi japo si sana kama huku.

Kama umesoma unaweza kujaribu kuulizia kazi za ofisi, bado wanaouhitaji wa wataalam. Wengi wa nguvu kazi zinazotumia brain si wazawa. Wengi ni wazimbabwe ndo wanaijenga Namibia.

Wako strict sana na issue za visa ili wakuruhusu kuingia na kukaa kwao.

Kuhusu hela wanatumia Namibia Dollar au Rands za South Africa ambayo ni one by one. Pili unaweza kwenda na US dollar utabadilishia huko. Wakati wa kubadilisha lazima uwe na passport yako na utakatwa commission % flani ya hela unayobadilisha.

Note: Kule life liko juu sana na issue ya accommodation ni expensive. Kuhusu hela wanatu
Maelezo yapo sawa kuhusu Namibia. Unaweza kupata kazi zile za kufanya kwa kichwa kwani kama udaktari na utaalamu mwingine mkubwa lakini kazi za mikono itakuwa shida kidogo
 
Hali imekuwa mbaya mpaka tunafikiria kuwa wazamiaji ili tutoke kimaisha. ASANTE TANZANIA YA AWAMU YA MSEMA KWELI.
 
Hali imekuwa mbaya mpaka tunafikiria kuwa wazamiaji ili tutoke kimaisha. ASANTE TANZANIA YA AWAMU YA MSEMA KWELI.
watu wanatafuta maisha bora kwa kuondoa iyo mbaya unayo isema...
 
mkuu mimi nawaza kwenda sychellies au mauritius ni kila ulaia wa mauritius nadondoka monaco kama naenda zenji... na monaco to ufaransa ni kugusa hivyo... nategemea kutafuta uraia tofauti na huu... maana hapa kwetu... tia maji tia maji hali si shwari... tuna umizana kwa makusudi nchi yetu sote lakini wengine wanatutumia kama matambala ya deki,,,, wana tuona kama wajinga .... ina kera sana....

tuta rudi kama wawekezaji.... wakina payet, nani na wengine wametokea tulipo wameenda walipo... na sisi tusonge mbele ndio maendeleo tusibaki hapa hapa na kulia lia tu wakati fursa si lazima hapa nchini tu

Mkuu huko sychellies nako kuingia hamna longolongo au
 
sychellies ni kisiwa hivyo ni mwendo wa ndege... za waarabu au kenya airways... pia una omba visa una enda... ila mauritius ni pasi yako na nauli na pesa ya kumudu huko... kwa kuwa kwenda huko kutokea tz ni kama kwenda SA... visa ni baadae
 
Mimi nafikili mkuu jipange hapahapa nyumbani kwani kuna Fursa nyingi sana mkuu
 
Habari wakuu naomba msaada,

Nataka kuanza safari ya kwenda Namibia kwa njia ya basi.

Je inawezekana kwanza? Pili niwe na document zipi ili nisisumbuliwe njiani na niandae kiasi gani njiani na wanatumia hela gani huko?

Mwisho kazi gani za ovyoovyo naweza kupata fasta na mkoa/jimbo gani kuna fursa kubwa ya ajira huko Namibia?.
Ukifika nenda mkoa uitwao Otjozondjupa kafukuzie kazi ya kuhudumia wazee. Jichanganye tu mkuu juu kwa juu tofauti na hivyo jiunge na CCM.
 
Namibia miaka ya nyuma tulikua tunapaita mchanga wa chuma hapachimbiki kitu...anza safari Tunduma mpaka Lusaka tsh 40,000 na ukifika Lusaka zipo bus za moja kwa moja pale intercity nauli ni kama Tsh 100,000 mpaka Windhoek kupitia Sesheke kote huko sijui Namibia,Botswana life kwa wageni kuanza ni kazi kidogo South Africa mpaka kesho itabaki kuwa kiwanja inategemeana na umejipangaje na una fani gani...Mnamibia anaitamani SA nae...
Sesheke ,mazabuku border karima Mulilo.. piga hadi Rundu ,Grootfontein,Outwarongo mzee Windhoek hii
Ha ha ninacho cha kusimulia uzeeni
 
ila sasa mkienda huko msiwe mabazazi ili kusiwe na burn kwa wanao toka tz... ili wengine tuje... tupo njiani.... maana tuna target nyingi sana tuna tik moja moja ktk note buku... nakuona itakayo fanikiwa ifanyike
 
Back
Top Bottom