Msaada: Natokwa na harufu mbaya sana sehemu za siri

Pole sana bro. vipi una mchumba? kama huna Tafuta uoe kabisaa...
hata kuoa sina hamu kaka maana saikolojia yangu haijatengamaa maana huwezi jua lini moyo utasema basi kabisa.maana najawa na mawazo ya namna ya kukatisha uhai siku hizi.Ni vile tu nawaonea huruma wale wananitegemea na wamenisomesha.
 
Pole sana chalii...nakushauri pia karibu KCMC idara ya ngozi kuna dermatologists wazuri sana na pia kuna dawa nyingi sana za matatizo ya ngozi ....

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante ndugu though kwa clinical sina imani tena maanakila nikienda naishia kupata majibu mepesi tofauti naukubwawa tatizo. naomba kuuliza ni sababu gani inasababisha huku kwenye testkuna over heat? maana ndio hali hii inaambatana na hili.
 
Ushauli wangu huu

1) wote waliokwambia uwainbox au kuwa follow wafuate bila kusita huwenda wakawa na cha kukusaidia kweli kwani kwa tatizo lako hauna muda wa kuhofia utapeli hata kidogo.

2) Usichoke kumuomba mungu muombe na muombe bila kikomo huwenda yajayo yakafurahisha kwako.

3) Licha ya kuwa tatizo lako hata ukiwa msafi lipo palepale ila hivyohivyo jutahidi kuwa msafi, hii itasaidia atayekujaji vibaya harufu ajisute mbona msafi hivi.

4) Unapokaa nawatu hakikisha sehemu iko open kujajibanabana ili harufu isisikike sana.

5) Endelea kutafuta tiba za kuponesha tatizo hilo kwani tunaamini anayeponesha mungu ila awezi kukufanyia ukiwa umelala ndani (anapitisha mambo yake kupitia sababu).

NB: kuna nabii aliumwa ugonjwa kwa muda wa miaka mingi nimesahau ule ugonjwa alioza mwili nzima na kutoa harufu mpaka mtaa mzima waliama mji ila kitu pekee alichofanya kumuomba Mungu, kuto kumkufuru mungu na kitu cha mwisho subira (alipona na kuwa na muonekano mzuri, hivyo nakushauli kuwa na subira kama aliyokuwa nayo nabii huyu kwani kuna neema yake.

Mwisho

Kama tatizo lilikuja ghafra basi litaondoka ghafra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna uchawi wa kunuka usiombe urogwe mavi hakuna mwanaume atae kugusa nimekumbuka dada mmoja alirogwa mume wame kila akimsogelea anamsikia ananuka mavi basi alikua analia ila alihangaika kienyeji akapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha kuvaa boxa hewa iwe inazunguka maeneo hayo, ukiwa umekaa mahali weka utaratibu wa kulegeza mkanda hewa iingie na kutoka hutpata fangas, wala hutasikia harufu.
 
Nimeshangaa unaposema huwa unarudia suruali na boxer.

Asee kurudia boxer ni kosa kubwa sana. Hiyo tu inaweza kukuletea harufu za ajabu.
Suruali pia kama ndo utaratibu wako kurudia basi usirudie kwa mfuatano.
Yaani ukiivaa leo usiiva kesho itundike ipate hewa na uje uivae walau baada ya siku mbili.

Kitu kingine unapaswa kuoga si chini ya mara mbili kwa siku.

Pia unapojiitawaza jitahidi ujitawaze kwa sabuni basi kama waona harufu ni kali.

Kuna tatizo kubwa kwa sisi wanaume kutokijuiosha katikati ya makalio vizuri na hii hupelekea wanaume wengi kuwa na harufu kali makalioni au chini ya pumbu pale.
Acha uongo mimi navaa boxer wiki nzima sinaga harufu ata siku moja..!

Kuna tatizo hapo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mdogo wangu Enol. Naomba ufanye haya, ambayo binafsi nilifanya baada ya kupatwa na tatizo linataka kufanana na lako. Chukua Nazi 2 kwa kuanzia. Vunja na kuna Nazi zote kisha tengeneza tui. Liache tui mpaka cream ijitenge na maji. Kisha chukua hiyo cream jipake sehemu yote ya siri na pembezoni (kwenye mapaja).

Jipake vizuri kabisa asubuh mara baada ya kuoga, na uendelee na shughuli zako. Jioni pia jipake na lala kwa amani kabisa. Na cream inayobaki uwe unahifadhi kwenye jokofu.

Au kama unamfahamu anayekamua mafuta ya Nazi bila kuyachemsha, kachukue na ufanye hivyo. Nina hakika na naamini utapona vizuri kabisa. Pole sana.
 
Mkuu... Kama una mwili mkubwa yani ni bonge na una mapaja manene jitahidi kufanya mazoez ili upunguze mapaja mana mi awali nlikuwa na tatizo kama lako la kutoa harufu ila nilikuja gundua ni hali yangu ya unene hivyo nkaanza fanya mazoezi asubuhi na jioni hadi mwili wangu ulivyokuwa wa wastani pia kula matunda sana na maji mengi pia epuka kurudia boxer jitahidi kubadili kila baada ya kuoga na usivae nguo uliwa mwili wako una maji...

A m a i z i n g E a g l e
 
Hali hii nimeipata ndio naingia u teenager just 14yrs old. kosa kubwa kama ni kufanya labda ilikuwa kuwa bright darasani ndio nahisi.sikuwa na demu wala tukio lolote la kuchukua cha mtu.hali imeendelea mpaka leo na huzidi kadri mda unavoenda.
Pole sana ndugu yangu, naamini huku utapata msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauli wangu huu

1) wote waliokwambia uwainbox au kuwa follow wafuate bila kusita huwenda wakawa na cha kukusaidia kweli kwani kwa tatizo lako hauna muda wa kuhofia utapeli hata kidogo.

2) Usichoke kumuomba mungu muombe na muombe bila kikomo huwenda yajayo yakafurahisha kwako.

3) Licha ya kuwa tatizo lako hata ukiwa msafi lipo palepale ila hivyohivyo jutahidi kuwa msafi, hii itasaidia atayekujaji vibaya harufu ajisute mbona msafi hivi.

4) Unapokaa nawatu hakikisha sehemu iko open kujajibanabana ili harufu isisikike sana.

5) Endelea kutafuta tiba za kuponesha tatizo hilo kwani tunaamini anayeponesha mungu ila awezi kukufanyia ukiwa umelala ndani (anapitisha mambo yake kupitia sababu).

NB: kuna nabii aliumwa ugonjwa kwa muda wa miaka mingi nimesahau ule ugonjwa alioza mwili nzima na kutoa harufu mpaka mtaa mzima waliama mji ila kitu pekee alichofanya kumuomba Mungu, kuto kumkufuru mungu na kitu cha mwisho subira (alipona na kuwa na muonekano mzuri, hivyo nakushauli kuwa na subira kama aliyokuwa nayo nabii huyu kwani kuna neema yake.

Mwisho

Kama tatizo lilikuja ghafra basi litaondoka ghafra

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante ndugu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom