Msaada: Nataka kujua nauli ya ndege kutoka Tanzania (Dar) mpaka Italy

mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,921
3,549
Habari wana JF,

Kuna ndugu yangu anataka kwenda Italy na kwa bahati mbaya hajui na wala mimi sijui bei ya nauli. Hivyo nikaona ni vyema niulize humu nikiamini kabisa kuna watu wenye ufahamu wa mambo mengi.

Ningeomba pia kujua mashirika na bei zake.
 
Posta mpya kama unaelekea Maktaba ya Taifa, kabla ya kufika Holiday In Hotel unakata kulia kuelekea YMCA, CITI BANK, DHL. Ukitoka YMCA mita kama 60 upande wako wa kulia kuna ghorofa yenye parking za magari, chini yake utaziona ofisi za Ethiopian Airlines.
 
Posta mpya kama unaelekea Maktaba ya Taifa, kabla ya kufika Holiday In Hotel unakata kulia kuelekea YMCA, CITI BANK, DHL. Ukitoka YMCA mita kama 60 upande wako wa kulia kuna ghorofa yenye parking za magari, chini yake utaziona ofisi za Ethiopian Airlines.
Thanks mkuu.
Nitafanya hivyo endapo nitakosa kabisa kujua nauli yake hapa kwenye mtandao.
 
Mwambie aingie kwenye mtandao, aende kwenye website ya shirika la ndege analotaka kusafiri nalo. Fanya booking ya safari yako. Ndio maana ya mtandao
Nashukuru kwa ushauri,ngoja nifuatilie kiongozi
 
Hili Shirika ni la kipuuzi sana,linafanya biashara kimazoea sana nahisi pia ndumba zinahusika maana haiwezekani wanatoa huduma mbovu lakini bado linakua tuu.
Nilipanda siku moja tukawa pale Bole int airport ni balaa tupu... service hovyo na wanaopanda pia hovyoo sana hiyo ndege ni kama yale mabus ya upendo ya Njombe ambayo abiria wake hupanda ba kuku kwenye bus!!
 
Usithubutu kupanda ethiopian ni hovyo sana... anaenda italy mji gani na lini? Safari ni ya kurudi au? Anarudi lini? Nijibu hayo maswali nikupe jibu
Mkuu Ethiopian Airline isingekuepo Africa ingelala sana unawezaje kuwadharau wenzetu wana 787 dreamliner karibu 10 kila moja ni usd 32 billion? ina jumla ya ndege 76 boeing na airbus za kutosha na fair zao za kawaida tuu..
 
mi naijua ya basi tu mkuu!

Nauli ya ndege inategemea mambo mengi:

1. Shirika la ndege unalotaka kusafiria, kuna tofauti kubwa sana kati ya Swiss International Airline na Ethiopian
2. Msimu unaotaka kusafiri.... Kuna tofauti kati ya msimu wa likizo i.e December na March- June
3. Njia unayotaka kutumia kununua tiketi yako- kununua mwenyewe au kutumia travel agent
 
Back
Top Bottom