Msaada; Natafuta kamusi ya lugha ya Kilatini kwa Kiingereza/Kiswahili

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Wakuu, huwa natamani kuifahamu lugha ya Kilatini lakini kwa kuanzia nikaona nitafute kamusi ya lugha hiyo, kwa bahati mbaya kwenye maduka makubwa kama Cathedral Bookshop Dar hakuna. Tafadhari mwenye kuelewa kamusi inapopatikana anitaarifu.
 
download..
 
Ushauri wa kwenda intaneti ni sawa. Kuna mambo mengi kupitia google.
Jaribu pia hapa:
Internet Archive Search: latin dictionary
Katika orodha angalia zile zenye download kama pdf, ikiwezakana pdf-black.

Unaweza kufanya vile pia kwa kitabu cha sarufi.
Internet Archive Search: latin grammar

Vilevile kwa lessons.

Unapoanza kusoma kumbuka matamshi ni kama Kiswahili, si Kiingereza.

Labda hii si vibaya kwa kuanza:
http://frcoulter.com/latin/First_Experience.pdf

Aude sapere !!
Mkuu, nashukuru sana kwa yote hayo. Taabu yangu ni kuwa kwa nini hapa nchini vitabu vya lugha hii havipatikani kabisa ila vya Kiingereza ni vingi tu?
 
Mkuu, nashukuru sana kwa yote hayo. Taabu yangu ni kuwa kwa nini hapa nchini vitabu vya lugha hii havipatikani kabisa ila vya Kiingereza ni vingi tu?
Naona si ajabu sana. Waroma wa Kale hawakufika hapa (wale waliofika KAMA walifika walikuwa Waroma kutoka Misri waliongea kati yao na kuandiki Kigiriki jinsi iloivyokuwa katika Mashariki ya Dola la Roma - soma kidogo hapa Periplus ya Bahari ya Eritrea - Wikipedia, kamusi elezo huru).

Lakini waliofika ni Waarabu, Wahindi na Waingereza walioacha nyayo za kilugha (Wajerumani walikaa muda kidogo tu, sijui maneno kutoka kwao ila Shule, Hela na "Dachi" kwa wale ambao bado wanaelewa neno hili)
 
Back
Top Bottom