Pole mkuu! Ila hukumu huwa inategemea na mahakama iliridhika vipi na ushahidi uliotolewa! Na pia kosa halisi alilotiwa hatiani muhusika! Mfano hapo kuna mambo matatu umeyasema kuhusu sakata hilo:
1.kuvunja nyumba
2.Kuiba vitu vyenye thamani ya 1.5
3.Kununua vitu vya wizi
Sasa hapo iwapo mahakama itajiridhisha kuwa mhusika hakuiba vitu, bali aliuziwa na mtu mwingine, hapo hukumu yake ni tofauti na mtu aliyetiwa hatiani kwa makosa hayo mengine ya kuvunja na kuiba vitu hivyo.
Pia ili mhusika alipe vitu vyote panahitajika pia kuthibitisha kwanza kuwa ni kweli ulikuwa mmiliki halali wa vitu hivyo vyote, hapo uonyeshe risit za manunuzi. Pia ithibitike pasipo shaka kuwa ni yeye aliiba vitu hivyo vyote, hapo ndipo mahakama inaweza kumtia hatiani kurudisha vitu hivyo vyote.
Pia lazima ieleweke kuwa kesi ya kumshtaki mtu kama mwizi ni tofauti na kesi ya kumshtaki mtu, kumdai akulipe alichokuibia!
Hivyo nakusihi kama bado una madai unayoweza kuyathibitisha , basi tafta mwanasheria akushauri nini cha kufanya katika rufaa utayoikata!
Wanasheria mnaweza kuongezea hapa.