MSAADA: Naombeni mnisaidie dawa ya jini kuuma

Naandika huu uzi nipo katika hali ngumu, tangu hasubuh sijaweka kitu mdomoni.

Jino linauma mpaka sijielewi kabisa. Nimetoka kuliziba juzi

Lakini maumivu ninayoyapata saiv hayasimuliki.

NAOMBA YEYOTE ANAYEJUA DAWA YA KULITULIZA ANISAIDIE NIWEZE HATA KUIONA HASUBUHI
Kaling'oe heri pengo kuliko jino bovu!usipende maumivu mkuu!hayana faida!
 
Kwasasa chukua maji ya vugu vugu weka na chumvi na kitunguu swaumu sukutua kidogo mara tatu baada ya dkk 5 tu litapoa mkuu
 
Pole sana mkuu,hilo jino litakuwa limezibwa vibaya rud hospital wakalitazame coz me nishawah zibaga halikunisumbua na mpka Leo lipo pouwah
 
Kuna dawa ya meno aka ya kuswaki inaitwa bright inasaidia sana hasa meno yaliyotoboka yanayouma.

Pole sana mkuu itafute itakusaidia.
 
Ninavyofahamu jino likikuuma sawasawa hutataka ushauri wa wala nini.

Unanyoosha hospital moja kwa moja kwenda kuling'oa.
 
Naandika huu uzi nipo katika hali ngumu, tangu hasubuh sijaweka kitu mdomoni.

Jino linauma mpaka sijielewi kabisa. Nimetoka kuliziba juzi

Lakini maumivu ninayoyapata saiv hayasimuliki.

NAOMBA YEYOTE ANAYEJUA DAWA YA KULITULIZA ANISAIDIE NIWEZE HATA KUIONA HASUBUHI
Nunua karafuu utafune halafu urudi hapa utoe ushuhuda,nenda maduka ya viungo vya vyakula utaipata hiyo karafuu
 
Back
Top Bottom