Hun, hii ni sensitive case, hivyo naomba nichangie kwa kirefu kidogo hoping I would be of help.
Suala la kuishi pamoja:-
Mahari ni small matter… Kuishi pamoja na mtu inapaswa sana kuangalia vitu vya msingi kwa kuweza kufanya maamuzi hayo. Else kama huyo mtu unaishi naye kwa majaribia na kwa malengo ya kuishi kwa muda mfupi tu.
Ila inapotokea mmesha amua mmeridhiana kuwa pamoja na kuishi pamoja (bila kujalisha kwa ndoa ama bila ndoa) ni muhimu sana kwa wazazi/ndugu or walezi wajue huyo mtu ambae unaishi nae sababu anything can happen. Inapotokea mtu wako hayupo serious, hataka or hana dalili yoyote ile ya kutaka kuonana na wazazi wako na hali mwaishi pamoja hadi mkafikia mmezaa – kwa mtazamo wangu naona hiyo ni ‘deal breaker' kabisa. Ni dalili tosha kuwa hakuchukulii serious…. Hivyo sishangai uliamua kuondoka. Na nikupongeze mana kweli hayo ni maamuzi magumu.
Suala la mtoto upande wako;
Najua inauma… Na najua ni ngumu mana hili lako nimewahi experience pia. Utakuwa unafanya makosa sana ikiwa hasira ulizo nazo kwa baba yake unazipandikiza kwa mtoto pia.
Hun umesema mwanao ana miaka mitano… Kweli mtoto wa miaka mitano agome kumuona baba yake hadi kulia? Kwamba baba yake huyo alivyokuwa anakutesa wewe (kama vile physical abuse) alikuwa anafanya mbele ya mtoto wake au na yeye pia alikuwa anamtesa?!
Wewe ndio una details zote, naomba jitahidi kutafakari hili suala la mtoto upya. Madhara ya kupandikiza mtoto mabaya kuhusu mzazi mwenzie ni yeye mwanao kukosa heshima na adabu dhidi ya watu waliomzidi. Akiwa na uwezo wa kumdharau mzazi wake (bila kujalisha ni mpuuuzi kiasi gani) itakuwa rahisi kwa wengine. Kwa mtoto mdogo kukosa adabu si kitu kizuri. Wacha akue atakuja tu kumjua mzazi wake kama kimeo ama laha… Akiwa tayari na uwezo wa kupambua mazuri na mabaya.
Ni kosa kubwa saana kuingiza ugomvi wa nyie kama wazazi kwa mtoto. Selfishness yenu kama wazazi humuumiza sana emotionally na psychologically pia.
Suala la mtoto upande wa Baba yake:-
Huyu ex wako hana mapenzi na mtoto wake… Mwanaume anaweza akakuchukia wewe na akakosana na wewe lakini si mtoto wake. Kuna wanawake wengine huvumiliwa na waume zao sababu tu ya mtoto/watoto walio zaa. Kwa maneno mengine ingekuwa si watoto hao huyo mama angekuwa kaachwa kitambo. Hivyo kitendo cha yeye kuacha kumuona mtoto kwa madai anaona uchungu ni wazi hana mapenzi na mtoto wake, ni mtu ambaye yupo so selfish na wala hana niya njema.
So kitendo cha kurudi sasa na kutaka kumtoa out na kwenda shuleni kumuona inaweza kuwa sababu ni hizi;
- Wewe anakutaka bado, hivyo anataka kutumia huyo mtoto ili arudiane na wewe.
- Katambua kuwa familia yenu haitaki yeye awe karibu na mtoto hivyo anataka kuwakomesheni.
- Anataka kudhihirisha kuwa hata kama hajafanya process hizo ambazo kaambiwa na mama yako ana uwezo wa kumuona mtoto.
*Hii inafanya kuonyesha hana adabu, heshima, busara wala hekima na he is not worth it. (Mtazamo wangu)
Msimamo wa Bibi mtoto:-
Upande wangu sioni kama anakosea…. Ana haki ya kusema hivyo. Mradi tu wewe uliweke wazi kwa mzazi mwenzio kuwa mama yako anataka kuwe na formalities na anaposema kumkomboa not necessarily kumaanisha yapaswa alipe gharama kubwa. Weka hasira pembeni kaa nae muongee kusuluhisha hili hasa kwa manufaa ya mtoto wako. Si lazima uwe naye but jengeni mahusiano ya toleration ya nyie kuwasiliana na pale inapo bidi yeye kumuona mtoto aweze kumuona but kwa mpangilio sawa.
Ushauri wangu
Hivyo bora mwambie awe mstaaarabu, afuate taratibu na kuwa kwenda shuleni kwa mtoto hakuleti picha nzuri kabisa maana mnawapa tu faida walimu hali hapo hapo mnamuumiza mtoto. Mwambie kwa uwazi kuwa kitendo cha yeye hapo kati kukata mguu kumuona mtoto, imefanya mtoto kupunguza mapenzi kwake... Vile vile mtoto bado ni mdogo kutolewa out bila wewe mama yake kuwepo, mana wamjua vema. Hiyo ni excuse tosha ya kutomtoa mtoto mana itabidi uwe wazi kuwa roho yako bado ni nzito huwezi kutoka naye out na mtoto hadi pale roho yako itakapo kuwa sawa. Huyo ni damu yake... Asifanye vitu kwa papara. Kama kweli anampenda na kumjali mwanae atafanya maamuzi ambayo ni manufaa ya mtoto na si kuwa selfish kwa kujiangalia yeye. Pia hapo ndipo pa kumbana kuwa mtoto si kumuona tu, na huduma pia ni muhimu.
Pole sana kwa kuumia. Najua ni rahisi kwa sie kutoa ushauri saababu haitugusi moja kwa moja ni watazamaji/wasikilizaji. Mwisho wa siku nakuombea uweze kufanya maamuzi ambayo ni sahihi kwako na mwanao pia. All the best.
Pamoja Saana.