Msaada: Naomba kujua tiba ya kukosa usingizi

seven vingt

Member
Oct 17, 2019
23
35
Habari wanajamvi,

Kwa muda sasa nimekuwa na tatizo la kukosa usingizi nimejaribu kuonana na baadhi ya matabibu wa afya ya akili akiwemo prof Ndosi nilipata matibabu.

Baada ya matumizi ya dawa napata usingizi lakini mchana nakuwa kama teja feeling sleepy all the day na nikiacha dawa hali ya kukosa usingizi inajirudia tena. Msaada kwa anaefahamu tiba sitapenda kuwa mteja wa sleeping pills.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi ni matunda na uji mida ya jioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikushauri unywe uji wakati wa jioni,hata mimi nikila chakula chepesi sana jioni usiku siwezi kulala.Usile kingi sana na pia usile chepesi sana.

Kingine unapaswa kuiombea hiyo hali ili Mungu akuepushie,inawezekana kabisa hiyo hali ikakuachia,nilikuwa na hiyo shida baada ya kuikabidhi shida yangu kwa Mungu wangu hatimaye ilikuja kuniachia na sasa hivi nalala kama mtoto mchanga, sio mchana wala usiku, ninaposema sasa nalala,huwa napata usingizi mzuri sana,sound sleep...
 
Hiyo inaitwa insomnia je kuna aina ya dawa zingine unatumia za magonjwa mfano PEP(post exposure prophylaxis),haloperido,benzhexol,amitriptyline au dawa zozote unatumia za kudumu? Je umeshawahi tibiwa au unatibiwa matatizo ya msongo au ugonjwa wa akili?

Je katika familia yenu mna tatizo au mtu viazi vyenu mna matatizo ya magonjwa ya akili? Je, una tabia za kulala mchana?

Kama yote hapana basi ondoa wasiwasi ila muone mtaalamu muhusika ila jitahidi usinywe kahawa au vinywaji vya caffeine kabla hujalala.

Pia tiba ya kienyeji pika mabiringanya kaanga na mayai ya kienyeji changanya kula kabla hujalala utalala usingizi wa pono.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia nilisahau kimoja jitahidi kuuchosha mwili kwa mazoezi au mazoezi ya faida mfano lima bustani au shamba mida ya jioni baada ya kutoka shughuli zako wakati wa jioni itakufanya ulale umechoka usingizi kwa binadamu ni muhimu angalau masaa sita.

Mtu asikudanye pombe inaleta usingizi inaitwa fictitious sleep ukweli hata ukilala lakini unaamka umechoka unatengeneza tatizo lingine kazini kwako kiufanisi.
Yote ni hapanaAsante kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu sijui dini yako ila kama mkristo we jaribu soma bible usiku wakati wa kulala usingizi unavyokujaga, shetani mwenyewe anauletea hatumi malaika wake kuonyesha jinsi h=gan hakipendi hiko kitendo..ukisoma novel poa tu.hutalala.
 
Hiyo inaitwa insomnia je kuna aina ya dawa zingine unatumia za magonjwa mfano PEP(post exposure prophylaxis),haloperido,benzhexol,amitriptyline au dawa zozote unatumia za kudumu? Je umeshawahi tibiwa au unatibiwa matatizo ya msongo au ugonjwa wa akili?

Je katika familia yenu mna tatizo au mtu viazi vyenu mna matatizo ya magonjwa ya akili? Je, una tabia za kulala mchana?

Kama yote hapana basi ondoa wasiwasi ila muone mtaalamu muhusika ila jitahidi usinywe kahawa au vinywaji vya caffeine kabla hujalala.

Pia tiba ya kienyeji pika mabiringanya kaanga na mayai ya kienyeji changanya kula kabla hujalala utalala usingizi wa pono.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba kujuzwa, je kutumia madawa ya ugonjwa wa akili kwa Muda mrefu inaweza sababisha insomia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajamvi,

Kwa muda sasa nimekuwa na tatizo la kukosa usingizi nimejaribu kuonana na baadhi ya matabibu wa afya ya akili akiwemo prof Ndosi nilipata matibabu.

Baada ya matumizi ya dawa napata usingizi lakini mchana nakuwa kama teja feeling sleepy all the day na nikiacha dawa hali ya kukosa usingizi inajirudia tena. Msaada kwa anaefahamu tiba sitapenda kuwa mteja wa sleeping pills.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu ni rahisi tu wai kuamka kama ni muislamu swali swala ya alfajir alaf ukitoka anza shughuli zako za kutafuta rizki matokeo yake unaporudi hone jioni oga kula nenda kaswali ishaa alaf nenda kitandani alaf uone km usingizi hautakupokea kwa smile
 
pole sana rafiki nilipatwa na shida hy pia nilipofiwa na mama yangu, so najua hali unayopitia...

Nikiwa katika hali yangu hy, nikawa nasikiliza redio free kipindi cha ndodi,akawa anazungumzia tatizo hilo na tiba yake,niliifuata na nikapona,nilikuwa nalala hadi nachukia.

Chuku bilinganya katakata vipande kama vya chips na viwe vichache tu vya kutosha labda sahani moja ya chipsi,usivimenye osha vizuri tu.
kisha gonga mayai mawili ya kuku wa kienyeji hafu tengeneza chipsi ya bilinganya,halafu kula,fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku 5,matokeo yake njoo utueleze hapa hapa

sijui sauti inatosha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajamvi,

Kwa muda sasa nimekuwa na tatizo la kukosa usingizi nimejaribu kuonana na baadhi ya matabibu wa afya ya akili akiwemo prof Ndosi nilipata matibabu.

Baada ya matumizi ya dawa napata usingizi lakini mchana nakuwa kama teja feeling sleepy all the day na nikiacha dawa hali ya kukosa usingizi inajirudia tena. Msaada kwa anaefahamu tiba sitapenda kuwa mteja wa sleeping pills.

Sent using Jamii Forums mobile app
.
 
Pendelea kufanya mazoezi hususani jioni.Mazoezi yanaleta usingizi mzuri.

Pia shika ibada.

Kama unatumia pombe acha.
 
Madawa ya akili yanaweza yakawa mojawapo ya sababu ya Insomnia. Jitahidi yafuatayo yanaweza kukusaidi

1. Epusha kuangalia vitu vyenye mwanga mkali masaa 2 kabla ya kulala

2. Amka mapema/alfajir na usilale tena mpaka mida ya kulala. Unaweza kusinzia(nap) mchana sio jioni na isizidi dakika 15

3. Fanya Ibada na mazoezi kadri iwezekanavyo. Jitahidi kusamehe na kusahau mambo hasi yote yaliyotokea mchana mchana

4. Hakikisha chumba unacholala kina
i mazingira mazuri.
ii Kinavutia kulala,
iii hewa ya kutosha inaingia na kutoka
iv hakina makorokoro mengi
v. Isiwe ni sehemu unayofanyia shughuli zako mchana
vi. Mashuka, matandiko na rangi za kuta ziwe rangi laini

5. Kuna musics/instruments laini laini kama ya Julio Iglesias unaweza ukafungulia saa kadhaa kabla ya kulala

6. Oga maji ya moto(waweza nyunyiza matone ya chapa ya shoka au Jivan San Jivan)na kuufanyia mwili massage na mafuta kama ya nazi

7. Epuka vinywaji vyenye Kafein, pombe na kama hivyo. Pendelea mchanganyiko wa Maziwa + Asali + Mdalasini. Ni dawa nzuri ya Insomnia.
Kunywa maji yasiwe ya baridi bali uvuguvugu au moto mengi kadri iwezekanavyo

8. Mwenza na mikito ni dawa kubwa ya usingizi

Nitaendelea sim inazingua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom