Msaada: Naomba kujua adoption laws za Tanzania

Jipu-bishi

Senior Member
Feb 16, 2016
105
103
Nianze kwa historia kidogo, mwaka 2007 nilimpoteza kakangu mkubwa na mke wake wote kwa pamoja kwenye ajali ya barabarani. Kwenye ndoa yao walifanikiwa kuwa na watoto wawili ambao walichukuliwa na mama yetu mzazi kuwalea. Leo hawa watoto mmoja darasa la saba mwingine darasa la Tano.

Xmas iliyopita niliamua kuweka box chini niende bongo kusherehekea xmas na familia. Baada ya dinner ya xmas mama akaniita na akawaita na wajukuu zake akawaambia "wajukuu zangu, baba yenu huyu hapa, kuanzia leo mjue mna baba na Mke wake ndo mama yenu" akanigeukia na mimi akaniambia, mwanangu, hawa ni watoto wako mimi niliwachukua tu kukusaidia ili umalize shule"
Maneno ya mama yaliniliza, kwasababu nimesomeshwa na wazazi wa Hawa watoto. Na sikutarajia kuwa watoto hawa wangekuwa bila baba na mama. Niliumia Sana kwa uchungu

Mimi Wakuu napiga box huku kwa Mzee Obama, naombeni kujua jinsi ya kuweza kuwaa adopt Hawa watoto ili niwachukue wawe wanangu, kwa Sheria za Marekani hakuna mgogoro kabisa Hilo linawezekana tena kwa haraka kabisa ila sifahamu kwa sheria za Tanzania nitaanzia wapi.

Naombeni kutanguliza shukrani
 
Pole sana kaka, kwa kuwa ni watanzania, anzia ofisi za ustawi wa jamii watakuelekeza. Nadhani itakuwa tofauti na anayeadopt mtoto ambaye siyo wa nduguye. Sababu zako za adoption kama ni kweli basi ni za msingi sana. Mkeo naye aridhie asije akawanyanyasa hao yatima Mungu atawashushia laana.
 
Asante Sana mkuu, maana humu usipoweka post ya mapenzi watu waipita tu mpaka wake wazee wa "Think Tank" ya JF sikuhizi wanakula emoji za kutosha tu kwenye hizo post.
 
Back
Top Bottom