Msaada: Naomba kufahamishwa sifa za mdhamini wakati wa kuomba kazi kwenye CV

SheriaE

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
606
446
Habari wakuu, poleni na majukumu ya kulijenga taifa.

Mimi ni mkazi wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Kulingana na kichwa cha uzi. Naomba msaada.

Kwa kifupi sifahamu au sina uhakika mdhamini anatakiwa awe vipi na niwe na mahusiano gani naye.

Swali lingine ni kwamba, ikiwa nimemuweka mtu kama mdhamini wangu kwenye CV ni lazima nimuambie au hakuna ulazima.

Pia ikiwezekana naomba mnianishie sifa za Mdhamini. Mfano nimeomba kazi Ajira Portal.

Natatizwa sana hapo. Msaada wenu wakuu nitafarijika. Mtaani kuna kaza

Good evening.
 
Ila hapo weka watu wowote wa karibu yako na contact zao,(hata washikaji wako) usiwe complicator kwenye vitu vidogo kama hivi Msomi kama wewe tena ukashindwa hata kula kuwazia wadhamini, inabidi uwaze pepa ya mchujo huko utumishi.

Kwa kuwa umeambiwa wadhamini watatu weka, huo mda wa kuwapigia Simu unadhani wanao, kikubwa fanya kinachotakikana.
 
Wadhamini ni wale watu wenye uwezo wa kutoa maelezo kuhusu wewe upande wa elimu na uzoefu wako katika kazi.
Wadhamini sio washikaji, wapenzi, wazazi hata kama wanaweza kutoa maelezo yako ya elimu na uzoefu wa kazi.
Asante kwa mchango wako mzuri, ubarikiwe.

Kwa mantiki hiyo ninaweza kuwaweka hata bila kuwapa taarifa kwamba nimewafanya kuwa ni wadhamini wangu?

Au ni lazima niwajulishe kwanza kuwa nataka kuwatumia kama wadhamini wangu.

Natanguliza shukurani.
 
Ila hapo weka watu wowote wa karibu yako na contact zao,(hata washikaji wako) usiwe complicator kwenye vitu vidogo kama hivi Msomi kama wewe tena ukashindwa hata kula kuwazia wadhamini, inabidi uwaze pepa ya mchujo huko utumishi.

Kwa kuwa umeambiwa wadhamini watatu weka, huo mda wa kuwapigia Simu unadhani wanao, kikubwa fanya kinachotakikana.
Asante
 
Asante kwa mchango wako mzuri, ubarikiwe.

Kwa mantiki hiyo ninaweza kuwaweka hata bila kuwapa taarifa kwamba nimewafanya kuwa ni wadhamini wangu?

Au ni lazima niwajulishe kwanza kuwa nataka kuwatumia kama wadhamini wangu.

Natanguliza shukurani.
Ni vizuri ukiwaambia.
 
Ni vizuri ukiwaambia.
Asante
Sasa kwa mfano nimesoma bachelor of arts in human resources management. Mwaka huu ndio nimemaliza
Je kwa hapo ni kina nani wanaweza kuwa wadhamini?

Je itakuwa ni sahihi nikiweka Lecturer wa kwanza, alafu aliekuwa supervisor wangu awe wa pili na mwisho nikaweka mchungaji wangu kule kijijini.
 
Hao Malecture ni sawa kuwaweka, tafuta mtu mwingine wa 3 angalau mwenye taalauma kama hiyo au anayefanya angalau kazi kama ya taaluma yako.

Hakikisha unawaomba wawe wadhamini wako kwa sababu wengine wanakubali na wengine wanakataa. Pia wengine wana utaratibu wao wa jinsi umuandike kuhusu cheo chake(yaani yeye ndio atakupa taarifa zake sahihi ambazo anapenda atambulike nazo).

Mwajiri akitaka kukufahamu zaidi atawapigia hao wadhamini ili awaulize kuhusu wewe, endapo umeweka mdhamini asiyekufahamu utatarajia akuelezee kweli akiulizwa?

Wadhamini wana mchango mkubwa wa kukutetea kwa kumuelewesha mwajiri akitaka kukujua zaidi.

Mfano uliwahi kufanya kazi sehemu X , sasa huyo msimamizi wako(boss) anakujua vizuri akiulizwa kuhusu wewe lazima akupambe kwa juhudi zako ulizonazo kazini.
 
Umemaliza kila Kitu boss
 
Weka za walimu wako from kindergarten to the date, weka pia kwa walimu wa kule ulikoenda field si una namba ya yule kiongozi mkuu,muombe kuwa nataka uwe shahidi wangu
NB akikataa achana nae kwakuwa list nu ndefu from kindergarten
 
Hao Malecture ni sawa kuwaweka, tafuta mtu mwingine wa 3 angalau mwenye taalauma kama hiyo au anayefanya angalau kazi kama ya taaluma yako.

Hakikisha unawaomba wawe wadhamini wako kwa sababu wengine wanakubali na wengine wanakataa. Pia wengine wana utaratibu wao wa jinsi umuandike kuhusu cheo chake(yaani yeye ndio atakupa taarifa zake sahihi ambazo anapenda atambulike nazo).

Mwajiri akitaka kukufahamu zaidi atawapigia hao wadhamini ili awaulize kuhusu wewe, endapo umeweka mdhamini asiyekufahamu utatarajia akuelezee kweli akiulizwa?

Wadhamini wana mchango mkubwa wa kukutetea kwa kumuelewesha mwajiri akitaka kukujua zaidi.

Mfano uliwahi kufanya kazi sehemu X , sasa huyo msimamizi wako(boss) anakujua vizuri akiulizwa kuhusu wewe lazima akupambe kwa juhudi zako ulizonazo kazini.
Shukurani
Kuna kingine, je hawa wadhamini huwa wanatafutwa baada ya kufuzu Usaili au hata kabla?
 
Asante
Sasa kwa mfano nimesoma bachelor of arts in human resources management. Mwaka huu ndio nimemaliza
Je kwa hapo ni kina nani wanaweza kuwa wadhamini?

Je itakuwa ni sahihi nikiweka Lecturer wa kwanza, alafu aliekuwa supervisor wangu awe wa pili na mwisho nikaweka mchungaji wangu kule kijijini.
Mchungaji mlikuwa mnasoma wote hr unaanza masihara sio 🙂
 
Shukurani
Kuna kingine, je hawa wadhamini huwa wanatafutwa baada ya kufuzu Usaili au hata kabla?

Mkuu Mwifwa amejitahidi kukuelimisha hapo juu; na yuko sahihi kabisa.

Wadhamini hawa ni watu ambao ni lazima wawe wanakufahamu vizuri tabia zako na sifa zako za kitaaluma. Wanaweza kuwa walimu wako waliokufundisha chuoni lakini wawe tu wanakufahamu vizuri na wawe tayari kuelezea sifa zako wakiombwa kufanya hivyo. Kwenye kazi siriazi mwajiri anaweza hata kwenda kuongea nao uso kwa uso badala ya maongezi tu ya kwenye simu.

Katika CV yako kule mwisho kabisa ndiyo yanakaa majina ya hawa wadhamini pamoja na habari zao zote za mawasiliano (namba za simu na emails zao). Kwa kawaida huwa ni watu watatu.

Inashauriwa sana usiweke tu ndugu zako au washikaji wa kijiweni lakini wawe watu wanaokujua kitaaluma kuhusiana na kile ulichosomea.

Hawa unakwenda na unawaomba personally kuwa unataka wawe wadhamini wako. Na hakikisha wanakukumbuka hata baada ya kuondoka chuoni (kama ni maprofesa wako). Hii ina maana kuwa ni lazima uwe na mawasiliano nao ya hapa na pale. Unaweza kuwa consistent kwa mfano kila mwaka wakati wa sikukuu za Krismasi au Eid unawatumia kadi ya kuwatakia mema ukijitambulisha wewe ni nani.

Ukiomba kazi (na ukapita kwenye mchujo) inabidi uwatafute na kuwaambia kuwa mimi ni fulani, ulinifundisha kozi fulani mwaka fulani na wewe ni mdhamini wangu. Nimeomba kazi mahali fulani na pengine waajiri watakuja kwako kuuliza sifa zangu hivyo nakupa heads up.

Na kwa vile wengi wao wanaweza kuwa bize sana basi unaweza ukajiandikia mwenyewe sifa zako za muhimu ambazo unataka wamwambie mwajiri wako mtarajiwa. Na wadhamini wengine watakwambia uandike hiyo barua yenye sifa zako mwenyewe halafu uwatumie na wao wataongezea tu vitu vichache kwa sababu wewe ndiyo unajijua zaidi kuliko mtu ye yote.

Recommendation letters nzuri kutoka kwa watu muhimu kama maprofesa wako ni kitu cha muhimu sana katika maombi yako ya kazi.

Mwaka fulani niliwahi kukaa kwenye selection committee ya shirika moja lililokuwa linatoa ufadhili kwa wanafunzi kutoka Afrika na recommendation letters zilikuwa zinachangia point 30 kwenye mchujo mzima. Unachukua recommendation letter kutoka kwa muombaji wa Nigeria, Kenya au Afrika Kusini unakuta ina kurasa tatu yaani imeandikwa vizuri sana mtu unasoma unapata picha ya mwombaji. Unachukua ya mwombaji kutoka Tanzania unakutana na " The applicant was a student in my junior Microeconomics class and he did well. I hope you will consider his application. Sincerely Prof. Ngwale." Ni wazi yule mwenye recommendation letters nzuri atapewa nafasi zaidi.

Naweza kukuongoza vizuri katika issues hizi na hata kukurekebishia CV yako ili iwe ya kimataifa zaidi ukitaka kwa sababu nina uzoefu wa kina na mambo haya.

Kila la heri
 
Back
Top Bottom