Msaada: Namtafuta Baba yangu

huyo Abbas sendeu ni mjina ya kondoa kiasili sendeu wanakuwaga kabila la kirangi, so huyo baba ako atakuwa ni mrangi wa huko kondoa!
 
Dah kwa makadirio huyo Sembeyu alisoma huko tengeru mwaka gani?
Alisoma pale kati ya mwaka 2006-2010. Ilikuwa amalize 2008 lakini akawa anakamatwa kamatwa sana! Hiyo ikikuwa wakati anasoma Diploma ya Afya tiba ya mifugo!
 
Toka lini mmeanza kutoa ushauri nasaha? Mi sijaona sehemu akisema ashauriwe afanyeje kuhusu yeye kutoambiwa na mama yake baba yake alipo.

ANAMTAFUTA BABA YAKE ACHEN SPECULATIONS ZISIZO ZA MSINGI.NO MATTER WHAT SHE HAS DECIDED TO LOOK FOR HER FATHER. MPENI USHAURI WA YEYE KUMPATA BABA YAKE.

Epukani kuwa watoa ushauri kwa jambo ambalo lipo clear. Anamtaka baba yake. Akionana naye ndo atafaham ukweli wote. Kuweni serious na acheni kujivika majukumu ambayo si yenu.
 
Ushauri murua
 
HILI NI NGUMU. DADA YANGU ALIZAA NA MTU NA KIJANA WAKE ANA UMRI WA MIAKA ISIYOPUNGUA 30. AMEKUWA AKIMSUMBUA MAMA YAKE MIAKA NENDA AMJULISHE BABA YAKE NA HATAKI. Ni ajabu sana. Afadhali angemwambia amekufa lakini hamjibu lolote. Wanawake ni wa ajabu sana. Halafu hata malezi mengi aliyapata kwa babu yake mzaa mama hivo hakumhangaikia sana kwa makuzi
 
Ukumbuke kua bado binti hajajua majina halisi/kamili ya babake
 
Mkuu kama maisha yanenda wachana na huyo dingi. Miaka 23 bado unahangaika kumtafuta?


Fanya mambo yako, achana kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.

Mimi kama ni kumtafuta ningekuwa namtafuta ili nimuondoe duniani sio kwa wema.
Niwie radhi kwa kukwambia: HUNA AKILI TIMAMU.
 
Amini amini nakuambia, katika huu msako wako kuna vitu viwil tegemea kuvipata; Utampata baba yako mzazi na Utampata Baba mzazi wa watoto wako.

Wote tuseme Aminaaaaaaaaaaa
 
Mnamhukumu tu mdingi bila kujua, vipi kama mama aliishia na ujauzito mzee hajui??? Vipi kama walivotengana mama alidanganya mtoto kadanja ili kupoteza ukaribu???yote yanawezekana amtafute tu ataujua ukweli kisha afanye uamuzi sasa.
Uko smart kichwani dada. Hongera.
 
Hatumii kilevi chchte
Tafuta ndugu wa karibu unaeona anaweza kua mbea mbea kidogo uwe unamnunulia zawadi zawadi mara kwa mara ukiona mumekua na ukaribu mkubwa mwambie akupe taarifa zinazoweza kusaidia kumjua babako.
Hilo likishindikana jaribu kususia hata chakula huku ukila kwa kujificha ili usidhurike, mamako/ndugu akiona umedhoofika labda wanaweza kukwambia kilichotokea kwa babaako.
 
Wakati mwingine, wa mama wanazingua ,nakumbuka kunajamaa flani huko huko tanga ila yeye ni ME alikuwa akimsumbua mama yake kuhusu baba yake na mama yake akawa anasema baba yako alianguka kwenye mnazi akafa,sasa jamaa ilikuwa akiuliza walipo mzika na vitu vingine bado anaona chenga kwa maana majibu haya ridhishi,
Ebwanaeee! Kumbe kuna ndugu alishikwa na huruma baada ya kuona jitihada za jamaa zinagonga mwamba(na hii ni kutokana jamaa alishtuka maana yeye ni kama singa singa na wadogo zake wote ni waswahili hata huyo baba anaemlea ni mswahili,ndomana akaamuakuuliza kwa nini yeye yupo tofauti na wengine na ndo maza akamjibu baba yako alianguka kwenye mnazi na akafa)
Basi bwana ndugu mwenye huruma akamtonya kuwa baba yako hajafa na baba yako anajua wewe ushafariki, na akamwambia mbane mama yako atakwambia baba yuko wapi
Daaaah! Hiyo siku jamaa sijui alikula mmea mana si kwa hasira zile(jamaa alikuwa dereva wa magali ya abiria),Alimshikia panga mama yaje mzazi na akamwambia nakupa nusu saa kama hutaniambia baba yupo wapi ...natenganisha kichwa na kiwili wili mana hata wewe ulishaniua kwa maneno yako.....Yaaani yule mama alitetemeka na akijikuta anamwambia kilakitu...Kuwa baba yako yupo Dar na ana miliki magari na ana asili kama ya kiarabu
Basi jamaaa akaja Dar kwa maelezo ya jina na sehemu akatafutaa wee! Mpaka akamuona babayake na mzee wake alifurahi sana sana kwa maana alisema alitoa mpaka pesa ya maziko ila akamwomba mwanae asemehe yote, Jamaa akawa ndokama anasimamia baadhi ya Mali za mzee
 
nimeipenda hii kali ya mwaka...
 
Ulifanikiwa kumpata mshua?
 
First pole kwa kumukosa baba yako, lakini niko na swali muhimu sana nataka kukuuliza JE MAMA YAKO MZAZI AKO HAI?? na kaa ako hai, mbona asikupe maelezo yote kamili kuhusu your dad? maana kulingana na vile nimesoma hii taarifa yako yaonekana wazazi wako ni watu wamesoma, walikuwa na elimu, so sio rahisi BINTI(mama yako mzazi) au kijana(baba yako mzazi) kutochukua taarifa za kule mwenza wake ametoka anaishi au mambo kaa hayo mkuu,mama zazi ako hai mkuu????
 
Pls naona wewe una akili dogo sana, dogo ametoa kila taarifa, mama walikuwa na baba, wanasoma, na kila kitu mambo ya kubakwa yanatokea wapi aki??? pls pls try try and reason a bit, good day sir
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…