Msaada: Namtafuta Baba yangu


Asante Dominica
 
Labda uelezee baba ako alikua anafanya kazi gani,sehemu gani pia elezea mama ako alikua anafanya kazi gani pia,
 
Kwa elimu yangu ndogo ya "ujasusi".Sendeu ni jina ambalo lipo kwa wapare,wasambaa na wazigua.Jambo la pili ni kuwa umetaja chuo cha biashara Shinyanga,hapo mdadisi mama akutajie mwaka na utaweza kujua baadhi wa watu waliokuwa hapo wakati huo na pia unaweza kwenda shinyanga na ukapta details zaidi.
La tatu,jaribu mitandao ya kijamii kama facebook na kulitafuta jina hilo,yatakuwa mengi lakini anza kuchuja taratibu na unaweza kubahatika.
La nne,katika dunia hii ujiandae kisaikolojia kwani unaweza ukapjua kwenu lakini usibahatike kumuona baba yako.
kila la heri usisahau kutupa mrejesho.
 

Ok thanks... ntashukuru sana utanichek kwa hiyo inayoishia 602 ndo nimetoka nayo
 
!
!
Mleta Uzi @samsha Hussein Nina Ushauri Mdogo Kuweza Kurahisisha Hii Kazi. Fanya Home Work Yako Kikamilifu Kabla Hujapost Huku. Tafuta Taarifa Za Awali Zinazojitosheleza, Mfano Ni Muhimu Kujua Jina Jina Kamili La Huyo Unayemtafuta. Ukipata Jina Trace Mahali Alipowahi Kuishi Au Kufanya Kazi, Fatilia Kwa Watu Wenu Wa Karibu. Yupo Mtu Atakuwa Na Clue Tu Whereabout Him.
 

Nashukuru sna nitaufanyia kazi huu ushauri wako..na kurudisha feedback
 

Ni sawa lakini miaka mingi tangu nianze kujitambua nmekuwa nikifanya hvyo bilaa mafanikio, pili hakuna ndugu yyte upande wangu anayeonessha kuijua au kushirikiana na mimi katika hili
 
kuna muda nahisi kuna kitu nafichwa kitu sasa ni mtu mzima nahitaji kufahamu ukweli ambao najua siwezi upata kwa mama zangu maana ni kipindi kirefu nimekuwa nikiungoja na kuutafuta
ionekanavyo kuna uadui mkubwa ulijitokeza baina ya babaako na mamako kiasi ambacho hawataki mkutane.nami natoa angalizo kwa wanaouliza maswali ya kijinga au yasiyofaa ukiona mtu kaja kuulizia kitu kanisani wakati anajua kinapatikana sokoni ujue kakikosa huko sokoni.toeni msaada badala ya kukebehi na kuzingua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…