Msaada: Namtafuta Baba yangu

Kwani nilikuwa nazungumzia furniture za zamani kwenye huu uzi? Acha Ujuaji na UBASHITE.
Tatizo ni kuvia kwako kwa akili ndo kunakusumbua,umevurugikiwa maono na umekosa kabisa uwezo wa kupambanua mambo.
 
Kama ulivyosema baba na mama waliishi pamoja kisha wakatengana! Nina imani kabisa mama atakuwa na detail kidogo kumuhusu baba, kaa chini na mama umuulize kwa utaratibu atakwambia. Kisha ulete mrejesho
 
Sasa wanini kama yeye hajawah kukutafuta
Unajua inawezekana baba alijaribu kumtafuta lakini wanavyohama ndio hajui wapo wapi. Wengi ya watoto hutafuta upande wa baba kwasababu ikitokea anahitaji mchango wa damu huwa rahisi kupatikana na kuchangia.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Kama ulivyosema baba na mama waliishi pamoja kisha wakatengana! Nina imani kabisa mama atakuwa na detail kidogo kumuhusu baba, kaa chini na mama umuulize kwa utaratibu atakwambia. Kisha ulete mrejesho
Tatizo usikute mama alibakwa na mjomba au baba ndio maana wanaficha ishu. Au hujawahi sikia baba au mjomba kambaka mwanawe?? Sasa kama hapo utamwabia vipi mtoto kama baba yangu ndio alienibaka na kukuza wewe au mjomba fulani ndio baba yako hatari sana.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Sikiliza Dada,mama yako huwezi jua nini kilipelekea akaachana na Baba yako,pengine sababu hiyo ndo inayomfanya hata ww akufiche kukueleza alipo Baba yako.

Hii inatokana na chuki ambayo aliijenga wakati huo na haijatoka na huenda isitoke. Shukuru Mungu hajakulisha hiyo sumu ya kukueleza ubaya wa Baba yako ukiwa bado mdogo.(mfano wa sumu km hiyo ni diamond plutnumz na mama yake. Diamond kutokana na kulishwa sumu ya chuki na mama yake dhidi ya Baba yake anamuona Baba yake takataka).

Cha kufanya,ulizia kwa mtego makazi yao ya mwisho wakiwa pamoja waliishi wapi,mtaa gani,walifanyakazi gani nk. Yaani hata ukijua tu kuhusu mama,inatosha sana,ukienda hayo maeneo lazima utapata pa kuanzia kujua mahali alipo Baba yako. Me nakuhakikishia,hakuna Jambo baya la kutisha kuhusu Baba yako,bali ni chuki tu za mama yako dhidi ya baba yako. Au yeye ndo alisababisha kutengana kwao,pengine kwa kufumaniwa hivyo hataki ufahamu juu ya hiyo aibu,maana anajua Baba lazima atakuambia. Kila la kheri Dada...!!
 
Hayupo tayari kuniweka wazi kuhusu hili swala sasa sielewi ni kwann ndo nimefikia maamuzi haya ya kuomba msaada wa taarifa kuhusu yeye

Kama mama hayuko tayari kukupa taarifa juu ya baba,chunguza kwa ndugu wa karibu na mama ama maeneo ambayo uliishi kipindi ukiwa mdogo lazima kuna watu wanaoweza kuwa na msaada
 

Dah! Ushauri mzuri sana umempa...haya Shamsa Hussein kazi kwako...
 
Mkuu kama maisha yanenda wachana na huyo dingi. Miaka 23 bado unahangaika kumtafuta?


Fanya mambo yako, achana kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.

Mimi kama ni kumtafuta ningekuwa namtafuta ili nimuondoe duniani sio kwa wema.
 
ni vp umehisi kuwa mm ni mbondei wa muheza?
Shamsa usijekuwa wewe ni mtoto wa Sendeu yule chitomb... tulikuwa naye chuo cha mifugo Tengeru? Ila jina la kwanza silikumbuki! Huyu jamaa ni kweli aliwahi kufanya kazi Mwanza idara ya mifugo kabla ya kwenda Arusha baadaye Dar manispaa ya Kinondoni. Hebu pitapita kwenye hizi manispaa zote za Dar idara ya mifugo, anzia kwanza Kino ukimkosa hapo nenda Ilala! Sendeu atanisamehe kama nimemchongea kwa binti yake aliyekuwa hataki amjue! Ila kama siye basi anaweza akawa babako mdogo au mkubwa! Nitakupigia simu leo tuelewane wewe mtoto wa Kibondei!!
 
Ongea vizuri na mama yako utampata baba yako.
Pili hujaweka full name ya mama yako
 
Tumia watu walio karibu na mama yako,has a mama yako Mkubwa au mdogo wamdadisi naimani atatoa siri,na ww utajua baba yako alipo, pia jitahidi kujisogeza karibu na mama atatoa Siri
 
Kwanza nakupa pole sana.. pili, umenitoa machozi gunia ndugu yangu najua unavyo umia kwa maandishi yako uloandika kwa msisitizo na huzuni moyoni... ongea na mama yakp kwa upole kwani hawezi kukuficha yoooteee mpe moyo na mpigie magoti ukiwa na huzuni huuu kma uloandika hapa huku ukitokwa machozi mengi.. nafikiri kwa cc wazazi huwa tuna huruma fulani...nn nakwambi hivyo walau wewe una mtafuta baba ila kuna wengine wasichana hawanaga hiyoo.. fanya kwa upole na mtangulize muumba wako asimamie hilo. Utafanikiwa.
 
Kuna watu wanachekesha na ushauri wao,mtu amekaa na mama yake zaidi ya miaka 20 ameshindwa kumpa hizo details then mnamshauri ambembeleze mama!
Yeye ndio anamjua mama yake na ndio maana amekuja humu baada ya kushindwa kumshawishi na kuna wale wanamwambia achana naye,jambo kama halijakukuta ni rahisi kuhukumu,sidhani kama anamtafuta ili amuombe msaada ila anataka kumjua ili amfahamu na aondoe hilo doa la kutomjua baba.
Kuna rafiki yangu baba yao alikua na mtoto nje na hakuwaambia ila jamaa alikuja akiwa mtu mzima baada ya kutafuta details za baba na akakaa kama masaa 5 tu baada ya kumuona mzee na family yake akaondoka na hakuacha details zozote alizuga atakuja tena.
Mpaka leo ni zaidi ya miaka 8 hawajui alipo na mzee wao alishafariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…