MSAADA: Namtafuta baba yangu Charles Muyumbilwa

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,399
Kwanza nitoe shukrani kwa member wote wa JF kwani kupitia uwanja huu wengi wamerudisha tabasamu baada ya kuonana na wapendwa wao.

Kama kichwa cha habari kilivyo ni kwamba.
Mimi UMBO CHARLES MUYUMBILWA(ke 26age) ninayeishi Mbeya Uyole ninamtafuta baba yangu ambaye kwa taarifa za mama ni kuwa waliishi Tanga muheza kijiji cha Maduma kwa kaka wa baba ambaye alikuwa askari.

Baba aliondoka kwenda masomoni dar mwaka 1994 akamuacha mama kwa bibi mzaa baba aliyejulikana kwa jina la SEKIDUMBA kijijini hapo MADUMA huko Tanga. Baba alimwacha mama akiwa na ujauzito wangu hapo kwa bibi.

Baada ya miezi kadhaa mama alijifungua mimi January 1995 na miezi michache mama aliondoka akarudi kwao Mbeya Usangu Mlangali kijiji cha Kutulo na kuendelea kuishi huko hadi sasa.

Nimesoma huku Mbeya nikilelewa na Mama yangu aitwaye Mariam Mjagala.

Inasemekana baba aliwahi kuja Mbeya kumtafuta mama ila aliishia mjini hakujua vijiji ambavyo tupo hivyo hakufanikiwa.

Naomba kwenu watanzania wenzangu mnisaidie kumuona na kumjua baba yangu hata kama alikufa basi nijue ndg zake na alipozikwa na kama ni mzima basi anione mwanaye nami nimuone.


Mawasiliano 0747 525 891 UMBO CHARLES MUYUMBILWA.
 
Dunia kwa sasa ni kijiji, jaribu kupata details zaidi kwa mama yako, Baba yako alisoma shule gani, ni kabila gani na kijijini kwao ni kijiji gani?

Natumaini ukiongezea hizo details ni rahisi kupata taarifa zake dead or alive.

Good luck.
Huyo baba ni mbena ila wazazi ndiyo walihamia Tanga huko kwa ufupi kuhusu elimu ya baba yake hajui lolote hata hizi taarifa kazidokoa kwa mama mzazi tu.
 
Mama wa huyu binti alishaolewa kwingine na pia huyu binti kiuchumi ni ngumu kufanikisha hilo.
Kweli nchi yetu ni shida tupu. Halafu hawa wanasiasa wanavyotumbua fedha utadhani hakuna mwananchi mwenye shida. Na hali ilivyo ngumu huyo baba yake kama siyo mtu wa busara, akisikia hali yake ya uchumi ni mbaya namna hii anaweza kukausha.
 
Kweli nchi yetu ni shida tupu. Halafu hawa wanasiasa wanavyotumbua fedha utadhani hakuna mwananchi mwenye shida. Na hali ilivyo ngumu huyo baba yake kama siyo mtu wa busara, akisikia hali yake ya uchumi ni mbaya namna hii anaweza kukausha.
Huyu binti kalelewa na baba wa kambo lakini kama ujuavyo malezi hayafanani na hata sasa shughuli afanyazo anapata tu hela ndogo ambayo haiwezi kutosha kufanya utalii wa kumtafuta baba yake.
Ana imani akimpata baba basi atapata baraka stahili.
 
Back
Top Bottom