Msaada namna ya upatikanaji wa leseni ya biashara ya e-commerce

Msukule Msafi

Member
Oct 10, 2018
55
45
Habari wadau, naomba mwenye kufahamu namna ya kupata leseni ya biashara ya duka la mtandaoni tafadhali naomba anijuze taratibu zake na pa kuanzia nawasilisha
 
Msukule Msafi,
Salama, kwa kuanza lazima uanze kusajili biashara yako na katika kusajili unaweza kusajili ukiwa kama kampuni au kwa kusajili jina tu la biashara as Proprietorship, lakini itapendeza zaidi kama utasajili ukiwa kama Kampuni maana utakuwa na uwanja mkubwa wa kufanya shughuli zingine.

Ukikamilisha kusajili itakubidi uende TRA kwaajili ya TIN na kufanyiwa makadilio ya kodi, ukimalizana na TRA utakwenda kuomba leseni ya biashara na pia utaenda TCRA kwaajili ya kupata kibali cha kuendesha biashara ya mtandaoni

Karibu san mawasiliano ya haraka ni 0718887102
 
Leseni ya e-commerce inatolewa na Brela/ wizara ya viwanda na Biashara. Haina uhusiano na TCRA. Domain ndo unalipia TZNIC kama utatumia kikoa cha .tz

Otherwise kama unaduka tayari na leseni ya duka...na bidhaa unazouza mtandaoni ni zile zile za dukani kwako basi hauhitJi leseni yoyote.
 
Mkuu shukran nipo na system tayari (website + app) my idea ni kuwa na store kama ile ya ali expresa so mtu au mfanyabishara ataagiza kitu kutokea hapo then ataletewa ka address atakayo weka sasa nikawa najiuliza namna kukamilisha taratibu za lesen maana nataka nifanye kila kitu kisheria ... nawasilisha .

Back
Top Bottom