Msaada namna ya kuweka verification Instagram

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
Ndugu zangu naombeni msaada Kwa wenye ujuzi namna ya kuweka verification kwenye Instagram

Natanguliza shukrani
 
Mkuu kuna utaratibu wa kupata official verification kutoka kwa dawati lao wenyewe mfano unaomba verification ukiwa na wafuasi fulani i mean base ya mashabiki, unatambulika pia kazi zako zinatambulika.
 
'INSTAGRAM VERIFICATION BADGE' (BLUE TICK) NI NINI HASA?
Verified badge ni alama ya tiki ya bluu inayoonekana mbele ya jina la akaunti ya mtu ya Instagram. Tiki hii inamaanisha kuwa Instagram WAMETHIBITISHA pasi na shaka kuwa akaunti hiyo NI HALISI (authentic) na inatumiwa na mtu mashuhuri/ mtu maarufu/ brand ya kimataifa anayoiwakilisha. Wameiweka ili kuwasaidia watu kutofautisha kati ya akaunti halisi na fake.

ILI KUPATA HII 'BLUE TICK' VIGEZO GANI VINAANGALIWA?
Kwanza, NI LAZIMA uwe aidha ni Mtu mashuhuri (Public figure), Mtu maarufu (Celebrity), au Chapa (Brand). Kama wewe ni Rais wa Buza, sahau kuhusu hii kitu - endelea kupambana ufahamike zaidi, na jina lako liwepo kwa wingi mtandaoni.

Instagram wanataka ku-verify watu ambao ni muhimu na maarufu kiasi ambacho kuna akaunti fake nyingi zinafunguliwa kwa majina yao. Kama wewe ni mtu wa kawaida tu, hakuna sababu ya mtu kutumia jina lako mtandaoni - haihitaji degree kujua hilo. Kwahiyo, kwa mtazamo wa Instagram, hakuna sababu ya wao kuku-verify ikiwa wewe ni 'mtu tu'.

Kwa kifupi, ili akaunti yako iwe verified, zingatia haya;
  • Akaunti iwe HALISI (Authentic): Akaunti yako lazima iwe inamwakilisha mtu halisi, biashara iliyosajiliwa au kampuni.
  • Akaunti iwe YA KIPEKEE (Unique): Akaunti yako lazima iwe ndiyo pekee inayomwakilisha mtu au kampuni. Akaunti moja tu kwa kila mtu au shirika ndo inaweza kuwa verified, isipokuwa kama akaunti zinatumia lugha tofauti. Instagram hai-verify akauti zisizokuwa 'specific'.
  • Akaunti iwe IMEKAMILIKA (Complete): Lazima iwe public na ina bio, picha (profile photo) na angalau post moja. Kwenye profile yako usiweke 'link' za mitandao mingine ya kijamii.
  • Akaunti iwe INAFAHAMIKA (Notable): Akaunti lazima iwe inamwakilisha mtu anaefahamika, anaetafutwa sana mtandaoni, brand, au kampuni. Instagram huwa wanapitia vyanzo mbalimbali vya habari ili kuona kama jina lako linatajwa mara kwa mara.
Sasa, vipo vigezo vingine pia lakini kama hivi nilivyotaja hapo juu unakidhi - basi unaweza kujaribu bahati yako (Nasema kujaribu kwasababu unaweza kuwa unakidhi vigezo vyote na ukanyimwa blue tick vile vile). Fuata hatua hizi;

Verification Instagram.PNG


Ikiwa unahitaji msaada wa kina zaidi, 'namba yangu unayo - utanipigia'.
#Virus
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom