ukitaka kufuata procedures ni kama ifuatavyo:
1. uwe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya udereva (mafunzo ni mwezi 1 kwa VETA ada ni 187,000/= kwa vyuo vya private bei ni juu zaidi)
2. nenda ofisi za TRA chukua TIN (kama huna), ni bure
3. toa copy cheti chako cha udereva, TIN na kitambulisho (200/=)
4. peleka TRA hivyo vitu waambie unahitaji leseni ya udereva.
5. utatozwa 53,000/==>10,000/= kwa ajili ya kukata learner, 3000/= ada ya mtihani wa majaribio (kujaribiwa kama unajua kuendesha na unajua alama za barabarani na 40,000/= ni kodi ya leseni kwa miaka 3.
6. ukimalizana na TRA unaenda kwa traffic officer kujaribiwa, hapa ndo huwa kunachelewesha, manake kumpata wa kukujaribia ni ishu, kila ukienda unazungushwa unaambiwa askari wote wako bize...
7. baada ya kujaribiwa askari atakomenti kwenye form kwamba upewe leseni umefuzu mtihani..