Tupo wanachama 11 na katiba inayotuongoza ipochakwanza naomba kujua misingi thabiti na idadi ya wana chama hai katika umoja wenu...nitajua namna ya kukuelekeza.pili kila kikundi cha umoja chena dhana ya kusaidia kutatua matatizo mbalimbali huwa kinakuwa na viongozi na kamati mbalimbali ya kutekeleza maazimio ya chama..wajumbe hawa huongozwa na taratibu maalum.. kama katiba.je katiba hii tayari mnayo?
kama katiba ipo ambayo ni msingi mkubwa wa utekelezaji shughuri zote za kikundi...ni yawazi kwawajumbe wote?(nikimaanisha nikatiba yenye maridhiano)hii husaidi kulinda umoja wenu ili isitokee mjumbe mwingine akahisi mnaongoza kienyeji.
unapo ona maoni haya machache yana reflect na mpango kazi wa umoja wenu. waweza kunitafuta kwa number 0755229028.kwataratibu zingine kwaajiri ya usajiri
mpaka kwa mrajisi vyama vya ushirika nk.
Asante kaka kwa ushauri wako naomba nijue vizuri kuhusu hayo majina 9 ya wanabodi yanatokana na wanachama au?Mnatakiwa kwanza muuandae RASIMU ya Katiba ya SACCOS yenu,pamoja na vipengele vinavyoainishwa ktk Katiba za SACCOS ni pamoja na Jina LA SACCOS na Majina 9 ya Bodi ya Waanzilishi wa SACCOS,.Wakati JF tunaendelea kuvuta kumbukumbu nenda Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata yoyote ,muulizie Afisa Ushirika au Afisa Maendeleo ya Jamii ,azima Nakala ya any SACCOS au Fika Ofisi ya Halmashauri ,onana na Afisa Ushirika
Asante kaka kwa ushauri wako naomba nijue vizuri kuhusu hayo majina 9 ya wanabodi yanatokana na wanachama au?
Asante sanaMkiwa wanachama 11 au idadi yeyote chini ya 20 hamtakuwa na haki ya kuanzisha SACCOS bali mtaanzisha Pre-Cooperative group,mtapewa muda wa kuikuza kufikia sifa ya kuwa na SACCOS.
Kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya 2013 lazima muwe wanachama msiopungua 20,kuwe na uwezekano kukua kiuchumi.
Maelekezo sahihi mtafute Afisa Ushirika wa Wilaya/Manispaa au Jiji kulingana na mahali ulipo.Kikao cha kwanza cha kuanzisha rasmi SACCOS ni lazima Afisa Ushirika awepo.Maelezo ya hatua za kupita,kuchagua Bodi anzilishi,kuandaa masharti ya chama( katiba),na taratibu nyingine utaelekezwa na Afisa huyo.Yeyote aliyekuomba uwasiliane naye nje ya taratibu za kiofisi ninazokuelekeza anakudanganya.Hata mimi ninayekupa ushauri huu nikikuita nje ya taratibu nilizokueleza nitakuwa nakudanganya.Ni matakwa ya kisheria.
Hakuna gharama yeyote ya kukutana na Afisa Ushirika wa Wilaya uliyopo.Nawatakia mafanikio makubwa.