MWAUWASA ni taasisi ya kijinga na inawadharau sana Wananchi wa jiji la Mwanza

kanali mstaafu

JF-Expert Member
May 17, 2015
4,314
2,000
Naandika hii mada kwa uchungu sana. Mamlaka za juu ikiwemo wizara na ikibidi Raisi waingilie kati matatizo ya taasisi hii kwa kunyanyasa wananchi.. hizi ni baadhi tu ya kero kubwa za taasisi hii kwa wananchi;

1. Kuanzia nameneja wa kanda (HASA KANDA YA
NYAKATO) mpaka wasoma mita wamejawa na kiburi,
majivuno, kutosikiliza matatizo ya wananchi. Na hata
wakisikiliza hawashughulikii.

2. Huwa wanakata maji mara kwa mara na mpaka huu
muda ninaoandika hili chapisho, KANDA YA
NYAKATO haina maji kwa siku nne mfululizo na
hakuna taarifa rasmi juu ya hili.

3. Mita nyingi mbovu hawazifanyii marekebisho,
wasoma mita kutokufika kusoma mita kisha kubuni
data, kukata maji kwa mteja akidaiwa mwezi mmoja
hata kama ni sh 4,000 na kuja kutozwa faini ya sh
15,000 pindi anaporudishiwa maji.

4. Kitenge cha huduma kwa wateja hawapokei simu na
hata ikitokea wakapokea ukawaelezea shida zako
wanakwambia usubir hata masaa manne na ukija
kuwapigia muda huo anapokea mwingine na
kukwambia ueleze shida upya. Utazungushwa
hvyohvyo mpka utakata tamaa.

Hii ni taasisi ya umma inayoendeshwa kwa kodi za wananchi na inatakiwa iwasikilize na kuwahudumia wananchi ambao kimsingi ndio waajiri wao.
Pia tunaomba serikali kama inaweza iruhusu kampuni binafsi ku-supply maji katika jiji hili ili tuwe na choice

MKUU WA MKOA, WIZARA, WAZIRI MKUU NA RAISI
Tusaidieni sisi wananchi wa jiji la mwanza kutupa jicho huku idara ya maji, HASA KANDA YA NYAKATO.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom