Msaada: Nahitaji mtu wa kunifundisha gari

Ndugu kuwa muelewa.. gari usipoendesha muda mrefu unaloose control.. ndio maana kazi za madereva zinataka experience.. yaani asome veta mwezi mmoja ajue kisha akae mwaka mzima bila kugusa gari.. halafu asikosee kweli?
Kwamba hata kufuata barabara itakuwa shida mpaka aishi mtaroni? Nimemshauri aongee na bosi afanye mazoezi kwa kutumia gari ya kazi.
 
Hii imenifanya nicheke, kwa hiyo madereva wanaenda wapi na kuwaachia wachuuzi wa barabarani wajibu wa kuyasogeza magari yao?
 
The truth will set you free.

Mpelekee alichokuagiza then mwambie ukweli Kama zoezi ndo huna ataelewa because sio wote wanaokwenda kujifundisha wanamiliki magari.
Nitafanya hivyo mkuu
 
Kweli mkuu veta tunafata cheti tu ila gari kujua ngumu sana maana practical zao ni muda mchache sana
 
Hapana mkuu, nishafanya kazi nyingi sana kulingana na elimu yangu na pia sijawahi kuogopa kuacha kazi kikubwa ni maslahi gani napata kulingana na kazi nnayofanya.
Kuhusu umaskini ni kweli unaleta hali ya mtu kutojiamini, na sio umaskini tu hata elimu pia mfano nchi zetu za kiafrika hatujiamini kwasababu ni maskini na kiwango cha wenye elimu kubwa ni kidogo kulingana na wenzetu ulaya.
 
Nimekuonea huruma. Kama bado hujapata mtu. Nicheki nikupe namba za mwamba bosi wa garage. Atakufundisha bure tena hata kwa gari manual. Mchawi itakua kuweka mafuta. Tena yupo Kigamboni hukohuko.
Ubarikiwe na mungu akuzidishie palipo pungua
 
Kwa hiyo VETA wanawapa watu Vyeti na Leseni bila uwezo wa kuendesha gari? Ina maana vijana wetu wanapoteza pesa bure kusoma VETA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…