Msaada: Nahitaji mawasiliano ya bodi ya mkopo (HESLB)

Msaada: Nahitaji mawasiliano ya bodi ya mkopo (HESLB)

Madindula

Member
Joined
Oct 24, 2019
Posts
38
Reaction score
27
Mambo vp jamani.

Nahitaji no. au mawasiliano ya bodi ya mkopo (HESLB) kama naweza kuyapata au msaada wowote wa karibu kama naweza kuipata tafadhali...
 
Nenda kwenye tovuti yao utapata mawasiliano yao mkuu
 
Hawapokei simu wala kujib email fanya uende tu ofisin kwao pale Vetenary karbu na Tazara (daraja la mfugale)

Nakushaurinuelezenshida yako unaweza PATA mawazo mbadala humu wapo maafisa wa bodi.
 
yani watu wanafanya kazi kisela sanaa yani era hii mpaka uende kule ofisini kwao yani website yaoo kimeo sanaa kila nikitaka kuangalia salio inagoma kuingia hata ukireset inagoma mambo y ajabu sanaa hizi habari za kwenda mpaka tazara what if nikiwa nafanya kazi ruvuma siwezi pata huduma yyte mpaka nije tazara
 
0736 66 55 33 (WhattsApp); 022 550 7910 (Calls from any network); adcp@heslb.go.tz. mawasiliano yao walio andika kwenye website haya lakini piga uoone utaacho kutana nachoo si whatsapp si regular call
 
0736 66 55 33 (WhattsApp); 022 550 7910 (Calls from any network); adcp@heslb.go.tz. mawasiliano yao walio andika kwenye website haya lakini piga uoone utaacho kutana nachoo si whatsapp si regular call
Heslb ya mwaka huu hovyo sana,kitengo cha mawasiliano bure kabisa, wanafunzi wanashindwa kufanya applications kwani kipengele cha NIDA pdf file kinawasumbua sana na hakuna msaada naona wamefanya makusudi iliwasikamilishe maombi kwa wakati
 
Wanufaika wapya wa Mkopo zaidi ya elfu 20 HESLB 2022/2023 | Majina ya Waliopata Mkopo
Habari njema kwa waombaji wote wa mkopo wa HESLB, Allocation ya mkopo bechi ya kwanza sasa inapatikana mtandaoni kuangalia allocation ya mkopo Tembelea Tovuti ya HESLB ya Maombi ya Mikopo na Mfumo wa Usimamizi https://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/Olas

Nifanye nini nikikosa mkopo kwenye bechi ya kwanza HESLB?
Kuwa mvumilivu na subiri kwa sababu bodi ya mkopo inatoa majina ya waombaji wa mkopo waliopata mkopo kwa Bechi. Bechi za majina ya waliopata mkopo ni nyingi wakati mwingine hufikia tano au sita

Je nikisubiri hadi bechi zote za majina zikatoka na ikiwa sioni jina langu, nifanye nini?
Bodi ya mikopo hufungua dirisha kwa waombaji kukata rufaa kwa hivyo ikiwa unajiona kuwa una hoja, unaweza kukata rufaa
Je, nifanye nini ikiwa sipati mkopo baada ya kukata rufaa?
  • Lipa ada ya masomo na chakula cha kujifadhili na gharama za malazi.
Naweza kuomba mkopo huku nikiendelea na masomo?

  • Ndio mwaka ujao bodi itafungua dirisha jipya la maombi
Maswali baadhi ambayo naweza kukupa msaada angalau wa majibu kuendena na uelewa wangu
Je, iwapo nilikatisha(disco) masomo nifanye nini ili niweze kupata mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) Soma hapa

Je, ni lazima nifuate taratibu gani ili nilipwe mkopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB)?

Ili bodi ifanye malipo, mnufaika lazima afuate taratibu hizi

1. Mfadhiliwa lazima ajiandikishe kikamilifu katika taasisi ya elimu ya Juu, vinginevyo itamfanya akose sifa ya kupokea fedha hizo.

2. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) lazima ipokee maelezo ya ziada ya wanufaika. Jukumu la kutuma taarifa hizo ni la taasisi ambayo wamekubali Wanufaika na kuwasajili kikamilifu.

Nyongeza:

iwapo mnufaika wa mkopo atajiandikisha katika taasisi ya elimu ya juu ambayo ni tofauti na ile ambayo TCU ilipeleka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), mnufaika hatapokea fedha za mkopo hadi aombe kupangiwa upya au Kuhamishiwa mkopo.

Ikiwa mnufaika atabadilisha programu yake aliyoichagua awali, kiasi cha mkopo wake hakitabadilika hadi aombe kutengewa tena.

Mwisho, bodi ya mikopo Huendelea kufuatilia maendeleo ya mnufaika katika Vyuo vya Elimu ya Juu mara kwa mara ili kufanya uamuzi wa malipo.

Recomended Posts

 
Back
Top Bottom