Msaada: Nahitaji kutoka katika hii nchi

Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
635
1,000
Habari zenu ndugu zangu,

Natumaini mko salama kabisa na kwa wale wenye changamoto mbalimbali za kimaisha msikate tamaa kwani siku njema zi karibu.

Nijikite katika mada husika, ni mimi kijana wenu Merchante nimerudi tena hapa jukwaani.

Lengo kuu ni kuomba kusaidiwa & kupewa njia/namna ya kutoka katika nchi hii na ikiwezekana nje kabisa ya hili bara ili nikajipatie riziki yangu.

Nimepambana sana katika hii nchi, ni mikoa mitatu tu ambayo sijawahi kwenda kutafuta riziki ila bado najiona kabisa sifikii malengo yangu, huenda fungu langu la kupata liko huko hivyo acha nilifuate.

Hivyo basi, ninatamani na ninahitaji sana kwenda kutafuta nje ya hii nchi, niko na nia thabiti na moyo mkunjufu katika hili. So yeyote yule ambae anaweza kunipa A-Z za kufika nchi za watu huko namkaribisha kuchangia au hata PM.

Sichagui kazi, ila tu iwe kazi halali.
 
Sirdirashy

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
2,570
2,000
Mkuu ww nimuhanga mwenzangu nataka niende Canada au Germany Kwa njia za mawakala Tafuta mawakala ndugu KAZI zipo Ulinzi, KAZI za manispaa na mahotelini shida Corona Huko uendako unaweza ukakata Moto.
 
Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
635
1,000
Mkuu ww nimuhanga mwenzangu nataka niende Canada au Germany Kwa njia za mawakala Tafuta mawakala ndugu KAZI zipo Ulinzi, KAZI za manispaa na mahotelini shida Corona Huko uendako unaweza ukakata Moto.
Mkuu wewe umepata angalau kwanga wa kufika huko? tusaidiane ndugu yangu.
 
Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
635
1,000
Mkuu ww nimuhanga mwenzangu nataka niende Canada au Germany Kwa njia za mawakala Tafuta mawakala ndugu KAZI zipo Ulinzi, KAZI za manispaa na mahotelini shida Corona Huko uendako unaweza ukakata Moto.
Usihofie kukata moto Mkuu,hata hapa hapa Tz tunaweza kukata moto hata kwa stress tu. Acha tukapambane nacho.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom