Msaada: Nahitaji kikundi ili nipate bima ya afya ya NHIF

ichenjezya

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
1,010
1,118
Habarini wana JF,

Nahtaji bima ya afya ya NHIF kwa ajili yangu binafsi sipo kwenye ajira, nilienda NHIF nikaambiwa kwa mtu binafsi inatakiwa kama 1.5M hivi, lakini nikaambiwa kama nina kikundi kilichosajiliwa naweza kupata bima hiyo kwa 78,000/-, tatizo sipo kwenye kikundi chochote.

Naomba msaada kama kuna mtu anafahamu kikundi kilichosajiliwa anipe msaada ili nijiunge nao ili nipate hiyo huduma, nipo Dar.

Ahsante!
 
Hiyo ni kweli CRDB bank walikuwaga wanafanya ujanja walipewa nafasi kukata kwa vikundi ila wao wakawa wanakata kwa mtu yoyote jamaa walipojua bima zote zinasitishwa na hivi sasa hawatoi tena

Ushauri tembelea vikundi vya SACCOS vikivyo karibu nawe wanaweza kusaidia
 
Habarini wana JF,

Nahtaji bima ya afya ya NHIF kwa ajili yangu binafsi sipo kwenye ajira, nilienda NHIF nikaambiwa kwa mtu binafsi inatakiwa kama 1.5M hivi, lakini nikaambiwa kama nina kikundi kilichosajiliwa naweza kupata bima hiyo kwa 78,000/-, tatizo sipo kwenye kikundi chochote.

Naomba msaada kama kuna mtu anafahamu kikundi kilichosajiliwa anipe msaada ili nijiunge nao ili nipate hiyo huduma, nipo Dar.

Ahsante!

Tumia wote scheme uwe unachangia 20K kila mwezi upate bima .Mwisho wa siku unachukua pesa zako
 
Njoo ujiunge na Saccos yetu inaitwa Mchikichini Saccos ina program ya bima ya afya ya NHIF, ofisi zipo nyuma ya soko la mitumba karume
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom