Kwanza kabla ya mambo yote niseme kwamba mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania ila ni mtazania mpenda mabadiliko,lakini haya maswali yananisumbua sana na nashindwa kujua mwanasiasa yupi wa kuamini.
1.Hivi kuna nchi hapa duniani ina mabwawa mengi,mito mingi,madini ya uranium,makaa ya mawe,na gesi kama Tanzania lakini ina shida ya umeme?
2.Hivi kuna nchi hapa duniani ina misitu kila kona lakini wanafunzi hawana madawati na wanakaa chini?
3.Hivi kuna nchi hapa duniani ina mito kibao,mabwawa kibao,mvua za kutosha kama Tanzania lakini wananchi hawana Maji safi na salama??
4.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani ina wasomi wengi wenye vipaji na taaluma za kutosha kama Tanzania lakini kazi wanapewa wageni na raia wanapuuzwa?
5.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani ina madini ya kutosha mfano dhahabu,na madini ya kipekee kama TANZANITE kama Tanzania lakini wazawa wanakataliwa kuchimba na migodi wanapewa wageni
6.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani viongozi wanaiba lakini wananchi wanashangilia kama Tanzania?
7.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani ambayo wananchi wanauza kura kwa vitenge na Kofia kama Tanzania?
8.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani ambayo wananchi wanachagua viongozi kwa ushabiki wa vyama na majina kama Tanzania?
9.Hivi kuna nchi yeyote duniani ambayo wanasiasa wanahamia vyama vingine vya siasa baada ya kukosa nafasi za uongozi kwenye vyama vyao kama tunavyofanya Tanzania?
10.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani ambapo kiongozi akiwa upinzani ni mchafu lakini akihamia kwako anasafishwa kama watabzania wanavyofanya?
11.Hivi kuna nchi yeyote hapa duniani ina asilimia kubwa ya wanasiasa wenye elimu ndogo kama Tanzania
Hivi kuna nchi yeyote duniani yenye madini mengi na vivutio vingi vya kitalii lakini serikali inategemea kodi ya pombe na sigara kujiendesha kama Tanzania
Mwisho:
Kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba mimi si mshabiki wa chama chochote cha siasa,naomba ndugu zangu watanzania mnisaidie,Je ni chama gani cha siasa naweza kujiunga ili niweze kutimiza haki yangu ya msingi ya kupiga kura!?