Msaada: Mwanangu ana tatizo la kula chumvi

Msaada: Mwanangu ana tatizo la kula chumvi

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,300
Habari wadau wa Jf

Nina tatizo ambalo linanisumbua kwa mwanangu. Mwanangu anakula chumvi kupita kiasi, ana miaka mitatu kasoro.

Hii tabia ameirithi kwa Baba yake ambaye naye alikuwa anakula chumvi sana, awezi kula chochote bila chumvi na hata akila anasema asikii ladha ya hicho chakula, chapati anaongeza chumvi kila kitu chakula chake ukiweka chumvi ya kawaida anaongeza kama nusu kijiko mtu wa kawaida uwezi kuonja kitu anachokula.

Hii hali siipendi kabisa lakini cha kusikitisha Mwanangu naye karithi, Mtoto anatoroka anakimbilia jikoni unamkuta kachukuwa chumvi kamwaga kwenye sahani ametulia anakula, tunda lolote hali bila chumvi, kuanzia papai, parachichi mkate na kila kitu mpaka kuwe na chumvi la sivyo atalia sana. Kwa sasa tunaificha chumvi kuliko sukari

Nisaidieni Kwanza nifahamu chanzo cha tatizo hili na namna navyoweza kumnusuru Mwanangu
 
Watu wana mambo.... Nina huyo mdogo wangu akiandaa chai yake we hunywi, anajaza sukari huyo.

Wengine hapa siku haiishi bila kutafuna mchele mbichi, nimeshajitahidi kuacha lakini nashindwa
Watu wana mambo.... Nina huyo mdogo wangu akiandaa chai yake we hunywi, anajaza sukari hiyo.
Sukari ikizidi kiwango kwa mda mrefu italeta shida...

kuna dogo mmoja naye kabalehe juzijuzi tu hapa sasa akipika ugali anaweka sukari, yan ndy alivyo lazima uji aueke sukari ndy asongee ugali. Kashakua kero sana ila asikii!
Wengine hapa siku haiishi bila kutafuna mchele mbichi, nimeshajitahidi kuacha lakini nashindwa
Hii nayo kali..atakuja mwingine naye atasema siku haiishi bila kula ndizi mbichi kama 4 hivi!
 
Inaweza kuwa ni dalili ya ukosefu wa madini flani Mwilini hasa Iron inafanya mtu anakula vitu vya ajabuu ajabu so fanya kumpeleka hospital afanyiwe vipimo na kupewa matibabu lakini pia inawezekana ni GENETIC issue hapo sasa ndo balaaa...
 
Habari wadau wa Jf

Nina tatizo ambalo linanisumbua kwa mwanangu. Mwanangu anakula chumvi kupita kiasi ,ana miaka mitatu kasoro...
Mpeleke hospitali haraka iwezekanavyo akapimwe atakuwa ana ukosefu wa madini mwilini mwake. ukifanya dharau chumvi ikizidi mwilini itaharibu figo lake lisiweze kufanya kazi kisha na maradhi ya presha ya kupanda mwisho wake utamkosa mwanao fanya haraka mpeleke hospitali akapimwe.
 
Watu wana mambo.... Nina huyo mdogo wangu akiandaa chai yake we hunywi, anajaza sukari huyo.

Wengine hapa siku haiishi bila kutafuna mchele mbichi, nimeshajitahidi kuacha lakini nashindwa

Hiyo ya kutafuna mchele nikajua peke yangu kumbe tuko wengi!
 
Aisee Sijawahi ona wala kusikia hili ndio kwanza
Chumvi nilivyosiipend Mimi
 
Sasa kwa kuanza hakikisha anakunywa maji mengi maana chumvi inahitaji ku balance na maji
 
Habari wadau wa Jf

Nina tatizo ambalo linanisumbua kwa mwanangu. Mwanangu anakula chumvi kupita kiasi ,ana miaka mitatu kasoro .

Hii tabia ameiridhi KWA baba yake ambaye naye anakula chumvi Sana ,awezi kula chochote bila chumvi na hata akila anasema asikii ladha ya hicho chakula ,chapati anaongeza chumvi kila kitu chakula chake ukiweka chumvi ya kawaida anaongeza Kama nusu kijiko mtu wa kawaida uwezi kuonja kitu anachokula.

Hii Hali siipendi kabisa lakini Cha kusikitisha mwanangu Naye karithi ,mtoto anatoroka anakimbilia jikoni unamkuta kachukuwa chumvi kamwaga kwenye sahani ametulia anakula ,tunda lolote Hali bila chumvi ,kuanzia papai ,parachichi mkate na KILA kitu mpaka kuwe na chumvi la sivyo atalia Sana. Kwa sasa tunaificha chumvi kuliko sukari

Note:Huyu mtoto hakai na babake muda mwingi wanaonana Mara chache KWA hiyo usiseme kaona KWA babake ,hii Ni amerithi Kama ilivyo na ya kwake ndo kali zaidi.

Nisaidieni Kwanza nifahamu jioni Cha tatizo hili na namna navyoweza kumnusuru mwanangu
Mimi ni mtu mzima sasa lakini toka utotoni nilizaliwa kama mwanao. Yani chakula sikisikii ladha kabisaa kisipokua na chumvi ya kutosha. Ata kiwe kizuri vipi Ila chumvi ikiwa kidogo naona kama nakula karatasi.

Nimefuatilia mtandaoni nikagundua ni conditions tu baadhi ya watu wanazaliwa nayo kiingereza huitwa supertasters. Kwahiyo usifiche chumvi unamnyanyasa tu mwanao bure ndo alivozaliwa
 
Kwa kawaida mwili wa binadam ukikosa vitamin flani huwa unakulazimisha ule kitu flani ili kubalance, hivo mwache mtoto ale hawezi kupata madhara
Sio vitamin mzee mbona Mimi ndo nimezaliwa hivyo
 
Mpeleke hospitali haraka iwezekanavyo akapimwe atakuwa ana ukosefu wa madini mwilini mwake. ukifanya dharau chumvi ikizidi mwilini itaharibu figo lake lisiweze kufanya kazi kisha na maradhi ya presha ya kupanda mwisho wake utamkosa mwanao fanya haraka mpeleke hospitali akapimwe.
Sikutegemea mtaalamu kama wewe uwe na jibu la kukurupuka hivi
 
Mimi ni mtu mzima sasa lakini toka utotoni nilizaliwa kama mwanao. Yani chakula sikisikii ladha kabisaa kisipokua na chumvi ya kutosha. Ata kiwe kizuri vipi Ila chumvi ikiwa kidogo naona kama nakula karatasi.

Nimefuatilia mtandaoni nikagundua ni conditions tu baadhi ya watu wanazaliwa nayo kiingereza huitwa supertasters. Kwahiyo usifiche chumvi unamnyanyasa tu mwanao bure ndo alivozaliwa
Vipi kuhusu madhara

Nimecheka Sana Mana mtoto yupo addicted huyu

Nilikuwa napika nikamimina chumvi kwenye kuganja nikaweka kwenye chakula nikasikia mama lamba mkono

Leo kachukuwa chumvi nusu pakiti kaloweka kwenye maji kanye's yote

Tangazo la chumvi ya Neel hata awe usingizini lazima aamke asikiize huwa halimpiti kabisa na anafurahia hatar
 
😹😹😹 Anafuatilia hadi tangazo la chimvi mweeee, huyu mtoto kwao baharini huko itakuwa
 
Watu wana mambo.... Nina huyo mdogo wangu akiandaa chai yake we hunywi, anajaza sukari huyo.

Wengine hapa siku haiishi bila kutafuna mchele mbichi, nimeshajitahidi kuacha lakini nashindwa

Dalili kama hizo kwa kimombo huitwa ‘generational curse/family curse’ ila kama wewe ni mcha Mungu na siyo siasa kali wa dhehebu lolote la dini, tiba hupatikana huko bila malipo yeyote kabla au baada ya kupona na tena inakuwa ‘instantly. Mungu anatoa bure na mchungaji lazima atoe bure ila wenye karama hizi ni wachache saaana duniani na siyo rahisi kuwatambua.(it is not easy to recognize them)!
 
Hakuna sumu mbaya kama chumvi mbichi.Usipomkimbiza hospitali kwa ushauri zaidi utakuja kujuta!
 
Back
Top Bottom