Salaaam wana jamvi!!!
Kuna siku mtoto alikua analia usiku, alilia kwa muda mpaka usiku sana, baada ya kubembelezwa bila mafanikio mm nikambeba nikamchapa kidogo miguuni (chapa ya kitoto) akanyamaza baada ya muda mfupi na akalala.
Sasa tangu sku hyo mtoto akiniona anakimbia na kuanza kulia, hata kama alikua anacheza anaacha kabisa, hii kitu inaninyima amani sana.
Naombeni msaada wenu ktk hili, ni vp naweza kabiliana na hii hali?
Mtoto ana umri wa mwaka 1 na nusu
Ukitaka kuwa rafiki na mtoto basi unatakiwa na wewe ufanye mambo ya kitoto kama vile kucheza nae michezo mbalimbali ambayo itamfanya arudishe imani na kukuchukulia kama rafiki yake.
Kumletea zawadi za hapa na pale pamoja na kuwa na tabasamu muda wote ukiwa karibu nae hivyo kumfanya mtoto akuone ni mtu mzuri.
Sio baba unarudi nyumbani umekunja sura kam nyama ya GOTI mpaka mtoto anaanza kukutilia mashaka.
Mkuu WISE BOY Pamoja na hivyo Sheria haikurusu umchape mtoto tena wa mwaka 1 na nusu umevunja sheria kama ni ulaya nilipo mimi huku unakwenda jela na mtotoNi mtoto wangu wa kuzaa. Sikumchapa kihivyo kama unavyodhani mkuu, ni ile chapa ya kitoto tu kama anavyochapwa mtoto anaekataa kunywa uji