Sikiliza ushauri wa kumpa dawa ya minyoo.
Pia kuna uwezekano mkubwa sana hiyo ni nocturnal allergic rhinitis.
Yaani kuna uwezekano hiyo ni shida ya 'aleji' ya usiku itokanayo na shida ya dust mites, au allergens zingine kama sabuni za kuogea zenye marashi makali, lotion au mafuta mnayopaka wewe, mkeo au mtoto wakati wa jioni na wakati wa kulala.
Angalia sana usafi wa mashuka, mito na chandarua cha kuzuia mbu.
Je chumba anacholala mtoto hakina vumbi au unyevu unyevu?
Je hamuaniki nguo mbichi chumbani (nguo kama, taulo, chupi, n.k)
Je unatumia deodorant ambazo harufu yake inakaa muda mrefu mwilini na mnalala na mtoto kitanda kimoja kibongo bongo?
Je unamvalisha au kumfunika nguo nzito mtoto?
Je mtoto analala na nguo alizoshinda nazo mchana na kulowa jasho?
Je mtot anatokwa sana jasho na kulowanisha mashuka? Kama ndio mnabadilisha mashuka masafi kila siku?
Je mnasafisha, fua au kubadili foronya za godoro na mito mara kwa mara?
Je unaweka chumani nguo ulizovaa mchana na kupuliza marashi makali? Baadhi ya marashi yanaleta shida kwa mtu mwenye allergy na kumtoa mafua laini yanyo sababisha kukohoa.
Je jioni mnapenda kumpa mtoto chakula gani?
Kuna baadhi ya wazazi wanawapa watoto chakula chenye karanga, mayai ya kisasa(kama chipsi yai) au maziwa ya ng'ombe fresh au mtindi.
Vyakula hivi huwaletea shida ya allergy watoto wengi hasa waliozaliwa kuanzia mwezi wa kumi (Oktoba) hadi mwezi wa tatu(Machi) mwishoni, hawa wengi huwa na shida ya allergy. Kuna watoto wengine wana allergy ya kurithi tu.
Kuna wengine wana asili ya allergy inayosababisha mafua mepesi kuvuja na kwenda kwenye mfumo wa hewa hivyo kusababisha mtoto akohoe.
Dawa ya allergy kama hizi zipo hospital ni nyingi tu lakini dawa rahisi na makini ya kiasili ni tangawizi, unaweza kuongeza na limao na asali.
Kuhusu uchafu na jasho husababisha wadudu (vijidudu) vidogo waitwao dust mite kuzaliana kwenye mashuka na godoro.
wadudu hawa wakikung'ta husababisha allergy na infection kwenye mfumo wa hewa na ngozi, wakati mwingine husababisha pumu (asthma) kabisa hasa kwa watoto na wazee.
Dawa badili mashuka, foronya, safisha chumba, hamia nyumba kavu, usianike nguo mbichi ndani(chumbani) kupunguza tatizo la dust mites.
Usivalishe mtoto masweta na miguo mizito usiku hasa maeneo yenye joto yanamtoa jasho linalowesha nguo na mashuka au godoro na kuzalisha dust mites.
MPELEKE MTOTO HOSPITAL, MIMI NA WEWE SIYO DAKTARI.