Msaada mtoto anaumwa

The secretary

JF-Expert Member
Jan 14, 2012
4,149
2,536
Jamani nimempeleka hospital lakini wamesema hana kitu ila anachemka sana halafu anakuwa kama anaweweseka au kusisimka joto likipanda.kwa sasa anamalizia ant malaria (mseto)madokta nisaidieni ni dawa au ni kingine?
 
Homa si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa.
Homa inaweza kusababishwa na mambo mengi sana. Mathlani, kidonda tu kinaweza kusababisha homa kali.

Dhana ya kuwa homa inaletwa na malaria tu, siyo sahihi.
Mtoto mdogo hawezi kujieleza, yawezekana na matatizo katika sikio 'otitis media' au mkojo 'UTI' n.k

Ni vema umrudishe hospitali akafanyiwe uchunguzi wa kina kubaini sababu zinazopelekea joto la mwili kuongezeka.

Kuweweseka si dalili nzuri kwasababu homa inapozidi inaweza kusababisha hali hiyo. Na hali inaweza kwenda mbele zaidi na kusababisha dege dege 'convulsion'. Matokeo ya dege dege nayo pia si mazuri kwa afya na maisha ya siku za baadaye
 
matibabu hapa itakuwa ngumu. The best ni kupata opinion kutoka kwa daktari baada ya kumuona mtoto
 
mpeleke kwenye hosp ya maspecialist wa watoto,
inaweza kuwa si malaria ni tatizo lingine tu wao watakusaidia.
 
Mtoto? Peleka fasta hospitali, ka bdg wameshindwa nenda kubwa... Mtanzania mwenzetu huyo anatakiwa awe ktk hali nzuri
 
Homa si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa.
Homa inaweza kusababishwa na mambo mengi sana. Mathlani, kidonda tu kinaweza kusababisha homa kali.

Dhana ya kuwa homa inaletwa na malaria tu, siyo sahihi.
Mtoto mdogo hawezi kujieleza, yawezekana na matatizo katika sikio 'otitis media' au mkojo 'UTI' n.k

Ni vema umrudishe hospitali akafanyiwe uchunguzi wa kina kubaini sababu zinazopelekea joto la mwili kuongezeka.

Kuweweseka si dalili nzuri kwasababu homa inapozidi inaweza kusababisha hali hiyo. Na hali inaweza kwenda mbele zaidi na kusababisha dege dege 'convulsion'. Matokeo ya dege dege nayo pia si mazuri kwa afya na maisha ya siku za baadaye

Kidonda anacho kidogo kwenye kidole maspecialista hadi j.3 naweza pata msaada wowote juu ya kushusha hii homa?
 
Back
Top Bottom