Nimatumaini yangu kuwa wote hamjambo na mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku.ndg zangu naomba msaada kwa yeyote mwenye ufahamu juu ya hili anisaidie.wapendwa nina ndugu yangu ana umri kati ya 15,16 au 17,anaitwa shida,ambaye alichukuliwa kijijini ikola wilaya ya sumbawanga vijijini mkoa wa rukwa,na kuletwa mjini tabora kwa minajili ya kufanya kazi za ndani ,yaani house girl.kweli alianza kufanya kazi kwa takriban mwaka 1,ila ilipofika mwanzon mwa mwezi wa 6 nilipigiwa simu toka huko kijijini kwamba binti ametoroka nyumbani yaani tabora na ameelekea dar .nilifanya juhud juu ya hilo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polis ila mpaka sasa bado sijampata.ila leo nimesikia katika uchambuzi wa magazeti kukiwa na habari inasema ,binti toka sumbawanga atelekezwa dar na mumewe..naomba msaada wa kujua hiyo habari au hata jina la gazeti maana mi niko singda vijijin.