Mzalendo wa TZ
Member
- Sep 2, 2012
- 48
- 7
Ndugu zangu Wanajukwaa nilikuwa na hamu sana ya kuona mkopo umetoka kwa kuamini kuwa nitakuwa mmoja kati ya watu watakaobahatika kupata mkopo.Lakini baada ya kupitia majina ya watu waliopata mikopo naiona dunia chungu na kujiona kama mtu aliyetengwa na ulimwengu kwani ndoto zangu nilizozipanga kwa muda mrefu zimeyeyuka ndani ya dakika moja.Naomba kupewa msaada wa mambo makuu mawili kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo waliofikia elimu ya juu na wadau wengine wa elimu;
1.Je hayo yote ndiyo majina ya watu wote wa mwaka wa kwanza waliopatiwa mikopo?Au kuna majina mengine mengine yatatolewa?
2.Kama siridhiki na kitendo hicho cha kunyimwa mkopo ninaweza kukata rufaa na kushughulikiwa kabla ya tarehe za kufungua vyuo?Na taratibu za kukata rufaa huwa zinakuwaje?
Nitafuruhi sana endapo mtanisaidia kunipa maelezo ya maswali yangu katika kipindi hiki kigumu kilichonikuta katika maisha yangu.Mwenyezi Mungu awabariki.