Msaada: Mkopo wangu utakuwa chuo kipi?

Msaada: Mkopo wangu utakuwa chuo kipi?

Vicin

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2017
Posts
676
Reaction score
295
Habarini wadau.
Awali ya yote ashukuriwe Mungu mwenye kutuwezesha yote.

Nashukuru Mungu nimepata chuo, mwanzo nilikuwa kwenye majina ya watu wenye matatizo, baadae udsm wakanichagua katika approved selection na wakasema kwamba waliopo kwenye hii list hawana haja ya kuconfirm, Mzumbe nawo wakanichagua katika approved selection. Kwahiyo sikuwa na option ya kuconfirm chuo chochote.

Jana nashukuru Mungu kanisaidia jina langu limetoka kwenye listi ya wanufaika wa mkopo.

Swali linakuja kwamba, mkopo wangu utatumwa chuo gani?
Mwenye msaada tafadhali anifahamishe.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Angalia kiasi cha ada tuition fee uliyopewa kisha ulinganishe na ya vyuo vyote ulivyochaguliwa utapatajibu labda uwe umepewa Asilimia ndogo ndo utashindwa kufahamu,ukigudua kuwa umechaguliwa chuo Fulani wapigie simu kule ambako hakujaelekezewa mkopo wakufute chuo itafanikiwa
 
Vyuo vyote ni 1.3 million, ila wameniandikia 1.28 million.
Nashukuru, bt nasubiria server zao ziwe vizuri halafu niangalie tena.
 
Vyuo vyote ni 1.3 million, ila wameniandikia 1.28 million.
Nashukuru, bt nasubiria server zao ziwe vizuri halafu niangalie tena.
We pambana utafanikiwa huu ni mwaka wako wa mafanikio ndugu yangu
 
Halfu tafuta no za simu vyuo vyote uulize nichuo gani wamekuwekea mkopo .
 
Sijajua kwa mwaka huu majina yanatoka vipi, ila kwa miaka iliyopita kunatokea jina la mnufaika, Chuo alichopangiwa, kozi husika pamoja na kiasi cha mkopo alichopewa.
 
Sijajua kwa mwaka huu majina yanatoka vipi, ila kwa miaka iliyopita kunatokea jina la mnufaika, Chuo alichopangiwa, kozi husika pamoja na kiasi cha mkopo alichopewa.
Hawajaweka, wameweka jina, namba ya form four, na jinsia tuu.
 
Halfu tafuta no za simu vyuo vyote uulize nichuo gani wamekuwekea mkopo .
Inawezekana kubadili allocation ya mkopo kutoka Chuo kimoja kwenda kingine? kabla ya kuripot Chuo
Mfano huyo Mtu amepata vyuo viwili tofauti na kozi tofauti pie ameshapata mkopo tayari alafu akapelekwa kozi ambayo hajaipenda.....
 
Back
Top Bottom