Msaada: Mke wangu mvivu kupindukia!

Msaada: Mke wangu mvivu kupindukia!

Allah's Slave

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
562
Reaction score
46
Habari,
Mimi nimeoa na ndoa yangu ina miaka 7 sasa na tuna watoto wa 2. Nlimuoa mwanamke aliyekuwa kamaliza degree ambaye alikuwa home tu at the time anatafuta ajira.

Toka nimuoe hajawahi kufanya kazi yoyote ile yaani Goalkeeper mpaka leo na kutafuta kazi alisha acha. Mpaka leo hii mke wangu hajabadilika. Namlipa mshahara mwisho wa mwezi ambao ni sawa na kama 10k per day yaani (300k).

Kila ninapojaribu kumtafutia kazi anafanya kidogo tu anaacha. Huwezi amini hata umlazimishe vipi ajishughulishe mzito ile mbaya. Mi ni mfanyabiashara(Magari Makubwa) nimemuanzishia vimiradi through the years vyote kala mtaji.

Kuna kipindi alijaribu kusoma masters ya bussiness administration nkamlipia ada, nunua vitabu vyote alafu yeye akaamua kuacha baada ya mwezi tu Eti kuamka alfajiri hawezi.

Nkaja nkamuomba basi asome chuo ambacho atakuwa anaingia mchana nacho alishindwa.

Tatizo rafiki yake mkubwa ni mama yangu mzazi hivo kuna kipindi nlikata mshahara wake ili kumlazimisha afanye kazi akakimbilia kulia manyanyaso nikalazimishwa hela yake isiguswe na wazazi wangu.

Nkienda kazini namuacha nyumbani na home kwenyewe hafanyi chochote anaita tu housegirl. Yaani yupo yupo tu siku hadi siku. Nifanyaje ili hata nikianguka leo au kesho awe ni mama atakayeweza kusomesha watoto.

Alafu matumizi yake ya hela mabaya yaani hela yake mwenyewe ukimpa mwanzo wa mwezi kwenye tarehe 1 hiv basi ikifika tarehe 8 ujue alikuwa anaumwa.

Ila ni hela yake na hainunui hata nguo ya mtoto hivyo hainihusu.

Nifanyaje ajishughulishe?
 
pole sana slave. nafikiri uchaguzi ndio umekuangusha.huenda uliangalia sura yake nzuri (naasume tu maana ndio tabia zao). Hata hivyo, ni vema ukae nae na kumweleza umuhimu wa yeye kufanya kazi.pesa ulizonazo asidhani kuwa ndio amefika.itakuwaje leo ukifilisika? si atakukimbia atafute mwingine mwenye hela? ya mung mengi , japo siombei...kesho na keshokutwa 'ukamaliza kazi yako hapa duniani', ataishije? na kwa baadhi ya familia na koo, kama ukatangulia, wazazi na ndugu za mume humpokonya mali zote kwani wanajua kuwa wewe ndiye mzalishaji.atafanyeje? mweleze ukweli wote ili auone huenda akabadilika.pole na ninakuombea katika hilo.
 
Mkuu mshukuru Mungu huyo mke wako anakutunzia watoto wako na wewe anakutimizia mahitaji kama mke. Huko maofisini unakotana kumleta mke wako si kuzuri, kuna mambo mengi tunayaona na kuwafanyia wake za watu yasiyostahili. Kama hana munkari wa kazi au biashara au shule haina maana ni mke kilaza. Tafuta kitu atakachofanya kitakachokuwa na interest kwake. Lakini usimhukumu after 7 years, lazima kuna mazuri uliyaona kwake. Wewe ndio baba na kidume kwenye familia, kutunza familia ni jukumu na wajibu wako. La msingi waandalie mazingira mazuri wanao endapo Muumba ataamua kukuita mbele ya haki wangali wadogo. Tusifananishe wake zetu na wake wa marafiki zetu kwani hujui wao wanaumiza vichwa kwa lipi.
 
Kwani huko nyumbani ndio kuzuri?
Unafikiri akikaa nyumbani ndio yuko safe?
Tafakari.
 
Id yako inasadifu vya kutosha ulio yaandika... Sizani kama mwanaume mwenye misimamo thabiti na uzoefu na mkewe kwa muda wote uo, anaweza kuja lalamika juu ya jambo dogo kama hilo... Msimamo wa mwanaume na hamu ya kufanya maamuzi magumu ni funzo tosha kwa mwanamke yeyote yule hapa duniani.
 
Kwani huko nyumbani ndio kuzuri?
Unafikiri akikaa nyumbani ndio yuko safe?
Tafakari.

Mkirua sasa unadandia treni kwa mbele. Wapi nimesema nyumbani ndio kuzuri? Usichanganye ulevi na pombe tafadhali.
 
Mkuu mshukuru Mungu huyo
mke wako anakutunzia watoto wako na wewe anakutimizia mahitaji kama mke.
Huko maofisini unakotana kumleta mke wako si kuzuri, kuna mambo mengi
tunayaona na kuwafanyia wake za watu yasiyostahili. Kama hana munkari wa
kazi au biashara au shule haina maana ni mke kilaza. Tafuta kitu
atakachofanya kitakachokuwa na interest kwake. Lakini usimhukumu after 7
years, lazima kuna mazuri uliyaona kwake. Wewe ndio baba na kidume
kwenye familia, kutunza familia ni jukumu na wajibu wako. La msingi
waandalie mazingira mazuri wanao endapo Muumba ataamua kukuita mbele ya
haki wangali wadogo. Tusifananishe wake zetu na wake wa marafiki zetu
kwani hujui wao wanaumiza vichwa kwa lipi.

Dah Mkuu nimekukubali, mleta mada jaribu kufata ushauri wa huyu mkuu!
 
pole sana slave. nafikiri uchaguzi ndio umekuangusha.huenda uliangalia sura yake nzuri (naasume tu maana ndio tabia zao). Hata hivyo, ni vema ukae nae na kumweleza umuhimu wa yeye kufanya kazi.pesa ulizonazo asidhani kuwa ndio amefika.itakuwaje leo ukifilisika? si atakukimbia atafute mwingine mwenye hela? ya mung mengi , japo siombei...kesho na keshokutwa 'ukamaliza kazi yako hapa duniani', ataishije? na kwa baadhi ya familia na koo, kama ukatangulia, wazazi na ndugu za mume humpokonya mali zote kwani wanajua kuwa wewe ndiye mzalishaji.atafanyeje? mweleze ukweli wote ili auone huenda akabadilika.pole na ninakuombea katika hilo.

Kma huwa unasafiri na magali safiri nae,gali likiharibika mpe spana ya yeye ajue ugumu wa faranga
 
Amekaliwa na mashetani, Peleka kanisani akaombewe, ni kwenye kanisa linalohubiri wokovu sio kanisa ilimradi kanisa
 
Na wewe anza kumdanganya kwamba biashara haiendi mambo yamekuwa magumu hela ya matumizi ambayo huwa unampa anza kumpa nusu yake ili ajue kwamba maisha ni magumu ataanza tu kujishughulisha
 
kaa na mkeo .mweleze jinsi anavokukera na kukuchosha na hayo maisha yake! labda hajui kama yupo wrong as long anakula na kushiba.
kama ulishamweleza hakukusikiliza na kubadilika basi wewe cha kufanya achana nae fanya mambo yako kama hayupo vile!
 
Na wewe anza kumdanganya kwamba biashara haiendi mambo yamekuwa magumu hela ambayo huwa ya matumizi ambayo huwa unampa anza kumpa nusu yake ili ajue kwamba maisha ni magumu ataanza tu kujishughulisha
mume anakupa laki tano kwa wiki kazi unafanya siku nzima unalipwa laki tano na makato juu neti laki 3 ...kwa nini nifanye? nani hapendi kula bata dunia hii?
 
kaa na mkeo .mweleze jinsi anavokukera na kukuchosha na hayo maisha yake! labda hajui kama yupo wrong as long anakula na kushiba.
kama ulishamweleza hakukusikiliza na kubadilika basi wewe cha kufanya achana nae fanya mambo yako kama hayupo vile!

teh teh teh muda mwingne unajielewaga kumbe,ila ongera kwa ulicho kinena
 
Unastahili pole huyo mkeo kweli ni mzigo afadhali hata mtoto utamtuma ila huyo mkeo mmmmmmmmmmmm pole sana.
 
Back
Top Bottom