Msaada: Mke wangu hajaona siku zake mwaka na nusu sasa baada ya kujifungua

beek

Member
Sep 23, 2020
99
137
Mabibi na Bwana habarini, naimani mko wazima wa afya.

Naomba nisiwachoshe sana niende kwenye mada.

Mimi ni kijana wa miaka 34 nina watoto wawili ambao kila mtoto na mama yake ila huyu mke wa kwanza tuliachana.

Sasa kilicho nisababisha kuandika huu uzi ni huyu mke wa pili baada ya kujifungua tu mpaka leo ana mwaka na nusu hajaziona siku zake ilihali huyu mke wa kwanza baada ya kujifungua ulipita mwezi mmoja tu akaanza

SASA SWALI LANGU JE NINI KINACHOSABABISHA HIYO HALI?
 
Sasa kilicho nisababisha kuandika huu uzi ni huyu mke wa pili baada ya kujifungua2 mpaka leo ana mwaka na nusu HAJAZIONA SIKU ZAKE.
Je, anatumia njia yeyote ya uzazi wa mpango?
Mfano:
- Kijiti au sindano??
 
Kuna hali inawakuta baadhi ya Wanawake, wakiwa ananyonyesha hawapati hedhi, ila wakiachisha tu mtoto kunyonya hedhi inarudi kama kawaida.
Otherwise labda awe anatumie sindano au vijiti vya uzazi wa mpango
 
Sidhani kama kuna vipimo JF, labda kwa siku za baadaye. Ndugu mteja, tafadhali tembelea hospitali ama kituo cha afya chochote kilicho karibu nawe ili upatiwe msaada mzuri wa kitabibu na ushauri. Je una swali lingine tofauti na hilo!?
kuwa muwazi kwamb hujui
 
Ni hormone tu.

Hormone inayozalisha maziwa(sijui jina lake) inakuwa nyingi katika damu hivyo kusbabisha kukosa hedhi.
 
sasa kwann iwe baadhi tu
Mkuu, shukuru mkeo haoni siku zake wakati ananyonyesha. Mtoto hakatishwi sababu ya mimba za bahati mbaya. Hii inatokea kwabaadhi ya wanawake na ni hali ya kawaida. Labda akiachisha hapo ndipo kutakuwa na shids
 
Mabibi na Bwana habarini, naimani mko wazima wa afya.

Naomba nisiwachoshe sana niende kwenye mada....
mkuu pole sana kama Umejaribu kumtibia kwa dawa za hospitali hajapona zipo dawa za asili akitibiwa anaweza kupona na akapata hedhi yake kama kawaida.
 
Hiyo hua inatokea kwa mama ambae ananyonyesha kwa kile kipind cha mwanzon hua haon siku zake inatokea tu kama atanyonyesha bila kumpa mtoto chakula chochote hii pia ni njia ya uzazi wa mpango.

Lakini kama haoni siku zake kuanzia miezi sita tangu ajifungue kuna tatizo kwenye hormone kwaiyo ni vizuri kama atamwona dactari wa gyne
 
Baada ya kujifungua haichukuwi muda mrefu hivyo ,Mimi ilinichukuwa miezi minne wengine sita,KWA mwaka naaaa ni mdarefu Sana ,tafuta nba ya kumuona gyno
 
Habari,

Hii ni hali ya kawaida kwa mama aliyejifungua na akaendela kunyonyesha vyema. Wakati wa unyonyeshaji, mwili hutoa kichocheo kinachoitwa Prolactin, ambacho husaidia kwenye kuchochea utengenezaji wa maziwa. Kwa kadri unyonyeshaji unapofanywa vyema kichocheo pia huongezeka.

Kuongezeka kwa kichocheo hiki hutuma ujumbe hasi kwa vichocheo vinavyoandaa mji wa mimba na mayai. Matokeo yake mama huwa hawezi kupata siku zake.

Miili huwa na uwezo tofauti katika hili wengine huweza kupata siku zao lakini wengine huwa hawapati. Lakini pia kuna sababu mbalimbali kikubwa ni kiasi cha unyonyeshaji na mwili wa mhusika.
 
Ni Kawaida sana, ila kumbuka kula chakula cha usiku kwa tahadhari,Maana huijui siku wala saa ya Mama kubeba Tena kwasababu tayari kashavuruga mzunguko wa siku zake.
 
Hiyo Hali Ni kawaida kwa baadi ya wanawake wachache pindi wananyonyesha kutokupata siku zao mpk pale atakapokuja kumwachisha mtoto ndo mzunguko wake unarudi kawaida
 
Back
Top Bottom